Mbunge wa bunge la EALA,James Ole Millya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hoja hiyo iliyojadiliwa bungeni
Mbunge wa EALA kutoka nchini Rwanda ,Fatuma Ndang’iza akizungumzia hoja hiyo bungeni hapo
Mbunge wa bunge la EALA kutoka nchini Kenya ,Maina Karobya akifafanua kuhusiana na hoja hiyo iliyokuwa ikijadiliwa bungeni hapo .
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha .WABUNGE kutoka nchi ya Kenya na Tanzania wamejadili hoja juu ya uchangiaji wa michango ya fedha kwa nchi saba za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao umekuwa ukisuasua kwa kipindi kirefu sasa na kukwamisha utekelezaji wa bajeti ya jumuiya hiyo ambapo Tanzania imeonyesha kuchangia kwa asilimia 100.
Akizungumza katika bunge hilo linaloendelea mkoani Arusha , Mbunge wa Bunge hilo James Ole Milya amesema zipo nchi zinasuasua katika michango yao hali inayochangia kuzorota kwa swala zima la maendeleo katika jumuiya hiyo kutokana na watu wachache wasiopenda kuchangia kama ambavyo wanafanya wengine.
Ole Milya amesema Tanzania inachangia kwa kutoa michango na ushirikiano katika maswala mbalimbali ili.jumuiya iendelee kuwepo kwa lengo la kusaidia wananchi wa jumuiya hiyo.
Amesema sio kwamba fedha hizo hapa nchini hazina Kazi hoja yetu sio kwamba hazina Kazi hapa nchini au kwamba tuna hela nyingi tunajaribu kujiweka kwamba tunasema Jumuiya hii tunaihitaji kwa kuondoa fedha ambazo zingetengeza miundombinu mbalimbali katika sekta za Afya Elimu Barabara tunachukua kidogo na kuweka humu kwa kuwa jumuiya tunaihitaji na tumeiasisi na tumeipenda.
“Kikubwa tunachotaka sisi tunataka wenzetu na wenyewe waone faida ya kuwepo ndani ya Jumuiya EAC basi wasukume kwenye bajeti zao kwa kuondoa kidogo walichonacho huko kwenye nchi zao walete kwenye Jumuiya kwa sababu nao wananufaika nayo hiyo ndio hoja ya msingi, lakini tumeona baadhi ya nchi zimetoka nje ya Bunge kwa sababu ya diplomasia naomba nisizitaje kwa Sasa lakini utaona wale nchi zao hawachangii wanatoka nje kukwamisha hoja hii” amesema Ole Millya.
Mbunge wa EALA kutoka Kenya Maina Karobya na mwenzake kutoka Tanzania Dk.Abdullah Makame walitumia kanuni za Bunge hilo ambazo zinaruhusu kuahirisha baadhi ya vifungu katika kanuni za Bunge hilo katika suala la akidi wakizitumia kanuni hizo ili kupata hoja hiyo kuchangiwa na wabunge .
“Unajua swala la hawa wabunge kutoka nje ya bunge halileti mashiko kabisa Tunachotaka Sisi ni kuona nchi zote zinachangia ipasavyo kama ambavyo nch zingine zinavyochangia kwani wote wanufaika na jumuiya hii.”amesema .
Suala la michango ya nchi Wanachama ndani ya Jumuiya limekuwa mwiba Mkubwa kwa nchi ambazo zimeonyesha kutochangia fedha za uendeshaji wa shughuli za Jumuiya hiyo ikiwemo bajeti yake hivyo wabunge kuamua kulivalia njuga ili kuweza utekelezaji wa bajeti kwa nchi Wanachama kuendelea kuchangia kwa asilimia zote.