MKUU wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Peter Lijualikali,akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 7,2023 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya kukamatwa na kumhoji kwa kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Bw. Godbless Lema kwa tuhuma za kutoa kauli ya kuhatarisha maisha ya Mtendaji wa Kijiji cha Korongwe Forodhani, Francis Duma.
MKUU wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Peter Lijualikali,akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 7,2023 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya kukamatwa na kumhoji kwa kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Bw. Godbless Lema kwa tuhuma za kutoa kauli ya kuhatarisha maisha ya Mtendaji wa Kijiji cha Korongwe Forodhani, Francis Duma.
MKUU wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Peter Lijualikali,akiwaonyesha waandishi wa habari clip ya Video ya Matamshi ya kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Bw. Godbless Lema wakati akihutubia Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Korongwe Forodhani, Francis Duma.
Na.Alex Sonna -DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Peter Lijualikali amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya hiyo,(OCD) Kumkamata na kumhoji kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Bw. Godbless Lema kwa tuhuma za kutoa kauli ya kuhatarisha maisha ya Mtendaji wa Kijiji cha Korongwe Forodhani, Francis Duma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 7,2023 Jijini Dodoma,Mhe.Lijualikali amesema kauli hizo zilizotolewa na kiongozi huyo kwa mara nyingine zimesadifu kabisa hoja ambazo zimekuwa zikielekezwa kwao kuwa chama hicho kinafuga vikundi vya kufanya vitendo vya kiuhalifu.
Inadaiwa Oktoba 24, 2023, Lema akiwa kijijini hapo kwenye mkutano wa hadhara alitoa kauli yenye ukakasi inayosababisha ofisa huyo kuishi kwa hofu.
“Katika mkutano huo, mmoja wa viongozi hao wa Chadema anayejulikana kwa jina la Godbless Lema, alisikika na alionekana akitoa kauli za kuchochea mauaji kwa kuhamasisha vikundi vya ‘vijana na wanaume’, wa chama hicho wakatishe uhai wa Mtendaji wa Kijiji, Ndugu Daudi Ismail.,”Amesema Mhe.Mhe.Lijualikali
Amesema kuwa ,tangu siku hiyo, kumekuwa na sintofahamu kubwa kutokana na vitisho vya kutishia maisha yake, ambavyo vinaonekana ni kuanza kutekelezwa kwa maelekezo ya kauli hiyo ya Godbless Lema aliyowaelekeza viongozi, wanachama na wafuasi wake.
“OCD wa Nkasi namuagiza kuchukua hatua za kisheria mara moja, kufanya upelelezi dhidi ya uchochezi wa mauaji aliofanya Lema na kuhatarisha uhai na maisha ya watu na hali ya usalama katika eneo letu, hali ambayo inakwaza juhudi za wananchi katika kujishughulisha na shughuli za maendeleo.”amesema
Aidha ameongeza kuwa CHADEMA kinafuga vikundi vya kufanya vitendo vya utekaji na mauaji, kama ambavyo aliyewahi kuwa kiongozi wao wa juu kabisa, amekuwa akinukuliwa akisema kwenye vyombo vya habari.
Mhe.Lijualikali ametoa rai kwa viongozi kutotumia vibaya uhuru uliotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan wa kufanya mikutano ya kisiasa kwa kuwa wote wanawajibu wa kulinda amani ya nchi.
Fullshangwe blog imezungumza kwa njia ya simu na Mtendaji wa Kijiji hicho Bw. Ismail amekiri kupokea vitisho hivyo na kutoa rai kwa viongozi wa CHADEMA kuacha kauli za uchochezi.
‘Matamshi aliyotoa kiongozi huyo yamesababisha kufanya kazi kwenye mazingira magumu kutokana na eneo lake ni mwambao wa Ziwa Tanganyika kuna mwingiliano wa watu wengi na uvuvi haramu.”amesema Bw.Ismail
Januari mwaka huu Rais Samia aliondoa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa lililoduku kwa zaidi ya miaka saba tangu 2015.