Waziri wa EALA nchini Kenya ,Peninah Malonza akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa bungeni hapo.
Kiongozi wa wengi bungeni ,John Loisa akizungumza na waandishi wa habari bungeni hapo
Mbunge wa EALA ,David Senkok akizungumza bungeni hapo
Julieth Laizer,Arusha .
Arusha.Waziri wa (EALA) kutoka Kenya Peninah Malonza ameahidi kushirikiana na kuchapa kazi kwa weledi mkubwa wakishirikiana na wabunge wenzake ikiwa ni pamoja na kuipeleka jumuiya hiyo katika viwango vingine .
Ameyasema hayo baada ya kuapishwa katika Bunge hilo mkoani Arusha huku akisisitiza swala la wabunge kuhudhuria kwa wingi katika baraza hilo ili kwa pamoja waweze kusukuma maendeleo mbele na kuondokana na changamoto mbalimbali.
Malonza ameahidi kutoa ushirikiano kwani Taifa la Kenya lipo mstari wa mbele kutengeneza Jumuiya iende mbele kwa kushirikiana na Mataifa yanayounda Jumuiya hiyo.
Aidha amesema kuwa, atahakikisha bunge hilo linasonga mbele na kukaa kwa pamoja katika kutatua changamoto mbalimbali na hatimaye kuweza kuwa bunge la mfano .
“Nipo tayari kutoa ushirikiano kwa nafasi hii niliyopewa au majukumu nitakayopewa katika Baraza la mawaziri wa Jumuiya yetu kupeleka gurudumu la Mtangamano wa Afrika Mashariki”amesema Waziri huyo.
Naye Kiongozi wa wengi bungeni kaunti ya Kajiado nchini Kenya John Loisa amesema wamejifunza mengi kupitia Bunge la EALA baada ya kushuhudia kuapishwa kwa Waziri wao bungeni humo sanjari na bajeti ndogo ya nyongeza.
Amesema kwa kipindi cha siku mbili walizokuwepo bungeni hapo wameweza kujifunza swala zima la Umoja huku akiziomba nchi wanachama kulipa kipaumbele suala la wafanyakazi wa Jumuiya hiyo kutofanya kazi kwa mkataba na badala yake kuajiriwa.
” Ukiangalia wafanyakazi wa Bunge na wale wa Mahakama wanafanyakazi kwa mkataba pengine wanalipwa fedha nyingi huku wengine wakitumika kwa miaka 5 hadi kumi lakini ukiondoka inakuwa ngumu kupata ajira nyingine tungelipenda watumishi hao kuanza kuajiriwa na kupata mafao pindi wakimaliza ajira zao na kuondoa suala hilo la mkataba”amesema Loisa.
Hata hiyo amesisitiza suala zima la kuboresha soko la pamoja ikiwemo kutumia ukubwa uliyokuwa nalo la idadi ya wakazi wa Jumuiya hiyo takribani watu.
Naye Mbunge wa EALA, David Sonkok amesema kwa pamoja watahakikisha wanashirikiana katika kuhakikisha jumuiya hiyo inasonga mbele na kuweza kuweka mikakati inayotekelezeka na kufanyiwa kazi kwa haraka ili kuharakisha swala zima la maendeleo katika jumuiya hiyo.