Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Oktoba 31,2023 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya kukamilika kwa utafiti wa Viashiria vya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa mwaka 2022/2023, ambapo matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Desemba mosi mwaka huu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duninia.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Oktoba 31,2023 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya kukamilika kwa utafiti wa Viashiria vya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa mwaka 2022/2023, ambapo matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Desemba mosi mwaka huu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duninia.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama, wakati akitoa taarifa ya kukamilika kwa utafiti wa Viashiria vya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa mwaka 2022/2023, ambapo matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Desemba mosi mwaka huu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duninia.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama,amesema Matokoe ya Utafiti wa Viashiria vya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa mwaka 2022/2023, yameonyesha maambukizi mapya ya VVU yameendelea kupungua nchini kulinganisha na matokeo ya utafiti kama huo uliofanyika mwaka 2016/2017.
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 31,2023 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na kukamilika kwa utafiti huo ambao matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Desemba mosi mwaka huu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duninia.
“Matokeo kamili ya utafiti huo yanatarajiwa kutangazwa Desemba mosi mwaka huu, lakini ni vyema watu wakafahamu kwamba Tanzania imeendelea kupata matokeo chanya kwani idadi ya maambukizi mapya imepungua kulinganisha na matokeo ya utafiti kama huo wa mwaka 2016/2017.”amesema Waziri Mhagama
Aidha Waziri Mhagama ameeleza kuwa Mafanikio hayo ni matokeo ya jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha maambukizi mapya ya VVU yanatokomezwa nchini.
”Tanzania imefanya vizuri pia katika kufikia lengo la sifuri tatu ambazo ni kumaliza maambukizi mapya ya VVU, kuondoa vitendo vya unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya wenye VVU na Ukimwi pamoja na kudhibiti vifo vitokanavyo na VVU.”amesema Waziri Mhagama
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kujiandaa kupokea matokeo rasmi ya utafiti huo ambao umeshirikisha taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi kikiwemo Chuo Kikuu cha Columbia kutoka nchini Marekani.
“Utafiti huu sio wa kwanza kufanyika nchini, umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka mitano ambapo mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2016/2017 ukiwa na lengo la kupima juhudi za serikali katika kupambana dhidi ya VVU.
“Kwa sasa ni utafiti wa tano kufanyika na wa pili kufanyika kwa ngazi ya jamii ambao wa kwanza ulifanyika mwaka 2016/2017 ambao unasaidia kupima mwenendo wa VVU nchini, viwango vya maambukizi mapya na maendeleo katika kufubaza VVU katika jamii,”ameeleza Waziri Mhagama