Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Mhe. Togolani Mavura muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon jijini Seoul kwa ajili ya ziara ya kikazi.
………………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Dkt. Frank Rijsberman jijini Seoul nchini Korea Kusini.
Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mbalimbali wamejadiliana kuhusu
utayari wa nchi kuwa mwanachama wa GGGI na kushirikiana na taasisi hiyo kuijengea uwezo Tanzania katika kuandaa programu, miradi na mikakati ya kufaidika na fedha na uwekezaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (climate financing).
Aidha, Waziri Dkt. Jafo ameshiriki Mkutano Mkuu wa 12 na Kikao cha 16 cha Baraza la Nchi Wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Green Global Growth wenye kujadili masuala mbalimbali kuhusu hifadhi ya mazingira.
Taasisi hiyo ya kimataifa yenye makao makuu yake katika Jiji la Seoul nchini Korea Kusini, ina takriban wanachama 48 na kati yao sita wanatoka katika Bara la Afrika Afrika.
Katika hatua nyingine akiwa katika ziara hiyo ya kikazi, Waziri Mhe. Dkt. Jafo amepata nafasi ya kushiriki katika mkutano na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini.
Mjadala katika mkutano huo mada iliyoandaliwa ni fursa zilizopo katika nchi hiyo za mazingira ambazo Tanzania inaweza kunufaika nazo zikiwemo Biashara ya Kaboni (Carbon Credit), Uchumi wa Buluu (Blue Economy) na Udhibiti wa Taka (Waste Management).
Waziri Jafo yupo ziarani nchini Korea Kusini kwa ziara ya kikazi ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha ushirikiano katika masuala ya mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Hayo ni matunda ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akiimarisha diplomasia na mataifa mbalimbali duniani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Mhe. Togolani Mavura muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon jijini Seoul kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini kwa ajili ya kushiriki Mkutano Mkuu wa 12 na Kikao cha 16 cha Baraza la Nchi Wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Green Global Growth.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Dkt. Frank Rijsberman jijini Seoul nchini Korea Kusini ambapo wamejadili kuhusu utayari wa Tanzania kuwa mwanachama wa GGGI na kushirikiana na taasisi hiyo kujengewa uwezo katika kuandaa programu, miradi na mikakati ya kufaidika na fedha na uwekezaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akishiriki Mkutano Mkuu wa 12 na Kikao cha 16 cha Baraza la Nchi Wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya Green Global Growth (GGI) kilichofanyika katika Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini ziara ya kikazi ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha ushirikiano katika masuala ya mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Dkt. Frank Rijsberman jijini Seoul nchini Korea Kusini mara baada ya mazungumzo yao kuhusu utayari wa Tanzania kuwa mwanachama wa GGGI na kushirikiana na taasisi hiyo kujengewa uwezo katika kuandaa programu, miradi na mikakati ya kufaidika na fedha na uwekezaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Dkt. Frank Rijsberman (kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Mhe. Togolani Mavura (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Dustan Shimbo (wa pili kulia) na watendaji wengine wa Serikali mara baada kikao baina ya viongozi hao wawili.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)