Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza na Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali nchini Wakili Kiomoni Kiburwa Kibamba akiwasilisha maombi ya Darasa kwa Naibu Katibu Mkuu (Picha Atley Kuni).
Diwani viti Maalum Chausiku Hassan Salumu Diwani Viti maalum Halmashauri ya Shinyanga vijijini akipongeza juhudi za Serikali ya awamu ya Nne kwakutekeleza ahadi za Ilani ya Chama cha mapinduzi ya mwaka 2015-2020 kwa vitendo.
Naibu Katibu Mkuu akiongea na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Festo Dugange akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wakati wa Ziara hiyo.
Na Atley Kuni- OR-TAMISEMI, Mwanza
Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini, Wakili Kiomoni Kibamba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, amewakilisha maombi maalum kwa Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Dkt. Dorothy Gwajima akimsihi kumpatia darasa maalum kwa ajili yakutoa somo kwa watumishi wa Halmashauri hiyo namna bora yakuweza kupangilia rasilimali watu katika sekta ya Afya kwenye Jiji hilo.
Wakili Kibamba ametoa ombi hilo muda mfupi mara baada ya Naibu Katibu Mkuu, kutembelea Kituo cha Afya Igoma na kukagua miundominu kisha kuzungumza na watumishi wa kituo hicho sambamba na timu ya Afya ya Halmashauri, ambapo katika maongezi yake Naibu Katibu Mkuu alihimiza suala la uwajibikaji lakini pia matumizi sahihi ya rasimali pamoja na huduma bora kwa mteja.
Akizungumza na watumishi hao, Dkt. Gwajima alisema inashangaza unakuta kituo kimoja cha afya kinaelemewa na wagonjwa ili hali kituo kingine kilichopo karibu hakina mgonjwa na chanzo kikuu ikiwa ni huduma mbovu na kutokumjali mgonjwa. Lakini pia suala la mtu mmoja kung’ang’ania eneo alilopangiwa ilihali uapande wa pili unaelemewa.
“Ndani ya kituo kimoja unakuta Muuguzi anasema mimi nimepangiwa wodi ya Mama na Mtoto kwaajili yakuzalisha, lakini ndani ya kituo hicho hicho upande mwingine mathalani wa wagonjwa wa nje wagonjwa wamejaa na ukitazama unakuta mtoa huduma huyo amezidiwa na hana msaada wakati yule wa wodi ya wazazi yeye yupo tu anasubiri mama aje ajifungue hili halina afya hata kidogo na ni matumizi mabaya ya rasimali watu” alisema Dkt. Gwajima.
Mara baada ya darasa hilo Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza hakuficha furaha yake na badala yake akaomba somo kama hilo angependa lifundishwe kwa watumishi wote wa afya wa Halmashauri hiyo kwa muda maalumu na ndipo alipo wasilisha maombi yake.
“Mhe. Naibu Katibu Mkuu, tumekuelewa sana, sasa mimi naomba niwasilishe maombi maalumu, nikuandalie darasa japo uje wewe na jopo lako unifundishie watu wa Halmashauri hii kwakweli naomba sana sana” alisihi Wakili Kibamba.
Kufuatia maombi hayo Naibu Katibu Mkuu alimkubalia ombi hilo na kuahidi kurudi katika Jiji hilo kwaajili yakwenda kutoa somo kwa watumishi hao.
Kituo cha Afya Igoma kituo kilicha anzishwa mwaka 1982 na nimiongozi mwa vituo vilivyopo katika Jiji la Mwanza ambacho kinauwezo wa kuhudumia watu 41,293 na watumishi wapatao 62 na katika mwaka wa fedha 2017/18 kilipatiwa fedha na serikali milioni 400 kwaajili ya upanuzi kwa majengo ya upasuaji, wodi ya wazazi, jingo la maabara, jingo la mionzi, jingo lakufulia sambamba na jingo lakuhifadhia maiti, ambayo yote yamekamilika kwa kujali thamani ya fedha na hivyo kumfurahisha Naibu Katibu Mkuu.
Naibu Katibu Mkuu yupo katika ziara ya kikazi kwenye mikoa ya Mara, Simiyu, Mwanza Shinyanga na Tabora ambapo katika ziara hiyo, amekuwa akitoa somo la matumizi bora ya rasimali watu na vitu lakini pia suala huduma bora kwa mteja.