Daktari Rose Chagama, mtaalamu wa Kifua kikuu na Ukoma kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke akielezea kwa kina kipimo kipya cha kikufua kikuu.
Temeke, Dar es Salaam
Kifua kikuu, ni moja ya ugonjwa hatari unaosababishwa na vimelea aina ya Mycobacterium tuberculosis,Visivyooneka Kwa Macho Hadi Kwa Hadubini umekuwa tishio kwa jamii kwa miongo kadhaa. Ugonjwa huu unaweza kuathiri mapafu na sehemu nyingine za mwili, na mara nyingi huchukua muda mrefu kugunduliwa kutokana na uelewa mdogo Katika jamii hivyo kupelekea kuchelewa kugundua tatizo mapema. Kifua kikuu kinagunduliwa Kwa njia ya upimaji wa Makohozi Kwa njia ya Hadubini na Vinasaba(Gene xpert) vipimo hivi ni Bure.
Hata hivyo, katika hatua ya kushangaza na ya kusisimua, Wizara ya Afya kupitia Mpango wa kutokomeza Kifua kikuu, wameongeza kipimo kingine Cha ugunduzi wa Kifua kikuu kwa kutumia haja Kubwa Kwa makundi maalumu ambayo ni Watoto chini ya Miaka 5 ambao hawana uwezo wa kutoa Sampuli ya Makohozi ,Wagonjwa wanaoishi na Maambukizi ya virus vya Ukimwi,na Wagonjwa waliolala Kitandani muda mrefu waliozidiwa.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke(TRRH) imeanza kutoa huduma za kiuchunguzi kwa wahisiwa(Presumptive) wa kifua kikuu kupitia kipimo hicho kipya. Ambacho kinatumia Vinasaba (Stool for Gene xpert) na kufanikiwa kugundua wagonjwa kadhaa ikiwemo mtoto wa miazi 5.
Dr. Rose Chagama, mtaalamu wa Kifua kikuu na Ukoma kutoka hospitali hiyo, anaeleza kuwa kipimo hicho ni kipya kwa Tanzania na kwa Temeke hospitali huduma imeanza kutolewa mwezi wa tisa mwishoni kuelekea mwezi wa kumi mwaka huu. Dr. chagama amesema kuwa, hichi kipimo cha Kifua kikuu kupitia Haja kubwa ni kipimo mahususi kwa makundi maalumu.
“Ni kipimo kipya kwa Tanzania na kilifanyiwa utafiti maeneo Kadhaa nakuthibitishwa kuwa kinafaa kutumika sasa wizara imeruhusu kitumike, hivyo Kwetu hapa temeke huduma hii imeanza mwezi wa tisa kuelekea wa kumi, na kipimo hiki ni kwa wale wahisiwa(presumptive) wa kifua kikuu, ambao wapo katika makundi maalamu kama vile watoto waliopo chini ya miaka mitano ambao hawawezi kutoa makohozi, wagonjwa waishio na Maambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na wale walioumwa muda mrefu na wapo vitandani hawajiwezi”
Aidha, Kupitia kipimo hicho itasaidia kuongeza ufanisi wa utoaji huduma na kupunguza vifo vya watoto waliopo chini ya miaka mitano na kwa wagonjwa waishio na maambukizi ya virusi vya ukimwi kwani Kifua kikuu ni moja ya Magonjwa nyemelezi yanayowapata na wengi kupoteza maisha Dr. Chagama amesema.
Hakika wizara ya Afya inaendelea kuboresha afya za wananchi kwa kuweka mazingira wezeshi ya kufanya tafiti mbalimbali zinazopelekea ugunduzi wa njia mbadala za kuimarisha Afya na kupunguza vifo Tanzania.