SIMBA SC imeshindwa kutamba katika uwanja wke wa nyumbani baada ya kufungana mabao 2-2 na Al Ahly ya Misri mchezo wa robo Fainali ya Michuano Mipya ya African Football League ambayo imezinduliwa leo katika Uwanja wa Benjamini Mkapa,jijini Dar Es Salaam.
Wageni walienda mapumziko wakiwa wanaongoza bao moja lililofungw na Reda Slim dakika ya 45 + 1 baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Simba SC.
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kufanya mabadiliko ya haraka haraka na kuendelea kuishambulia ngome ya Al Ahly ambao walikuwa wanacheza kwa kushambulia na kuzuia.
Simba walicharuka na kupata mabao mawili ndani ya dakika ya saba yakifungwa na Kibu Denis dakika ya 53 kwa pasi ya Clatous Chama,bao la pili likifungwa kwa kichwa na Saido Kanoute dakika ya 59.
Baada ya kufungwa mabao hayo mawili Al Ahly walitulia na kupata bao la kusawazisha likifungwa dakika ya 63 na Mahmoud Kahraba.
Kwa Matokeo hayo yanailazimu Simba SC kwenda kupata ushindi wa aina yoyote ili iweze kusonga mbele katika hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo Timu hizo zinatarajia kurudiana Oktoba 24,mwaka huu nchini Misri.