Afisa masoko mfuko wa huduma za Afya Zanzibar Asha Kassim Biwi a akizungumza na watendaji wa umoja wa watu wenye ulemavu kuhusiana na dhana ya mfuko huo huko Kikwajuni Mjini Unguja.
Afisa masoko mfuko wa huduma za Afya Zanzibar Asha Kassim akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji umoja wa watu wenye ulemavu Shaibu Abdalla mohammed karatasi yenye orodha ya Hospital zinatoa huduma kupitia mfuko huo.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Na Rahma Khamis Maelezo
Viongozi wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar wametakiwa kufikisha ujumbe kwa watu wenye mahitaji maalumu juu ya dhana ya Mfuko wa Huduma za Afya ili kuwajengea uwelewa.
Akizungumza na watendaji wa Umoja huo huko Ofisini kwao Kikwajuni Welless Afisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa vHuduma za Afya Asha Kassim Biwi amesema watu weye mahitaji maalumu wana haki kama watu wengine hivyo kupatiwa elimu hiyo itawasaidia kufahamu dhana ya mfuko huo.
Aidha amewashauri kutumia mbinu zao mbalimbali wanazotumia ili kufikisha ujumbe kwa watu wenye mahitaji maaalumu ili na wao wanufaike na mfuko huo kwa vile na wao wana haki ya kupata huduma bora za afya.
Amefahamisha kuwa katika hatua za awali mfuko umeanza kutoa huduma kwa waajiriwa wa Serikali na watotoambapo mchangiaji na watoto wake wa kuwazaa wameanza kupata huduma kupatia mfuko huo na baada ya kukamilika kuendelea na wafanyakazi wa Sekta binafsi
Hata hivyo Afisa huyo amewataka Watumishi wa Umma kuharakisha kukamilisha zoezi la usajili katika Mfuko huo ili kuwapa nafasi makundi mengine ikiwemo makundi maalum.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Shaibu Abdalla Moh’d ameushuku Uongozi wa Mfuko huo kwa kufika kwao na kusema kuwa watahakikisha kila mmoja uanapata taarifa hizo kwa njia moja ua nyengne kwani bila ya Afya hakuna maendeleo.