WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwa timu ya usimamizi wa huduma za Afya mkoa (RHMT) na Timu ya uendeshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo (HMT) leo mara baada ya kutembelea hospitali hiyo,kulia kwake ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo Dkt Rashid Suleiman akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali hiyo Dkt Joseph Mberesero
KATIBU wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Abasi Mlawa akimueleza jambo wakati wakati wa ziara yake alipozungumza na timu ya hospitali hiyo (HMT)
Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Abasi Mlawa kushoto akisisitiza jambo kwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Rashid Suleiman
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kushoto akimuonyesha Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Abasi Mlawa kulia eneo ambalo kutajengwa jengo la mama na mtoto katika Hospitali hiyo wakati wa ziara ya Waziri huyo leo katika Hospitali hiyo
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) katikati akisisitiza jambo kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Dkt Rashid Suleiman kulia ni Dkt Juma Ramadhani ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Matibabu ya Dharura katika Hospitali hiyo (EMD)
Na Oscar Assenga,TANGA
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo huku akiwataka watumishi wa Hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuhakikisha wagonjwa wanaokwenda wanapata huduma.
Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) amefanya ziara ya kutembelea kwenye hospitali hiyo ambapo pamoja na mambo mengine alizungumza na timu ya hospitali hiyo (HMT) ambapo aliwataka madaktari na wauguzi kuhakikisha wanatoa maelezo sahihi ya wagonjwa wanapolazwa na ndugu.
Amesema hatua hiyo itawaepusha kuwaondolea wagonjwa sintofahamu hususani wanapokuwa wakiulizwa na aina ya ugonjwa anaoumwa mgonjwa wake .
Akiwa kwenye mazungumzo hayo aliwataka watumishi wa Hospitali hiyo kufanya kazi kwa waledi mkubwa hususani katika kuwahudumia wagonjwa wanaofika kupata huduma za matibabu.
Hata hivyo amewapongeza watumishi kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa kuwatiaa moyo huku akiwataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea