Meneja wa Shirika la Bima (NIC) Kanda ya ziwa Stella Marwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya utekelezaji wa shughuli zao
Meneja wa Shirika la Bima (NIC) Kanda ya ziwa Stella Marwa akielezea umuhimu wa kuwa na Bima mbalimbali ikiwemo ya nyumba
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wananchi wametakiwa kukata bima za nyumba ili kuepuka hasara ambayo inaweza kujitokeza kutokana na majanga mbalimbali yanayoweza kuleta uharibifu kwenye nyumba ikiwemo mafuriko.
Wito huo umetolewa leo Jumanne Oktoba 17, 2023 na Meneja wa Shirika la Bima (NIC) Kanda ya ziwa Stella Marwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mwanza kuhusiana na shughuli mbalimbali wanazozitekeleza kuelekea kwenye hafla ya usiku wa wadau wa habari na waandishi wa habari iliyoandaliwa na Klabu ya waandishi wa habari Mkoani hapa.
Amesema bima za nyumba zinaumuhimu mkubwa sana hasa pale majanga yanapokuwa yametokea fidia inatolewa na mtu anaenda kujenga nyumba nyingine na maisha yanaendelea.
“Sisi kama NIC tunawasihi sana wananchi wakate bima za nyumba kwaajili ya kukinga nyumba zao ili hata mvua kubwa zinaponyesha na kuleta madhara wasipate hasara na kuanza kuiomba Serikali iwape msaada suluhisho la majanga yote ikiwemo ya moto,mafuriko ni kuwa na bima,na faida kubwa ya bima inaondoa mawazo “, amesema Marwa
Amesema wamekuwa wakiendelea kutoa elimu za bima katika sehemu mbalimbali ikiwemo kushiriki maonesho mbalimbali na makongamano kwaajili ya kutoa elimu hiyo.