NJOMBE
Kufuatia serikali kutoa muongozo wa kilimo cha parachichi ili kuongeza tija kwa mkulima na kuetengeneza soko la uhakika la ndani na nje ya nchi ,Wakulima wa parachichi maarufu dhahabu ya kijani mkoani Njombe wameomba serikali kudhibiti uzalishaji holela wa miche isiyo na ubora na kisha kusogeza huduma muhimu katika kilimo hicho ikiwemo Maji ,nishati ya umeme na barabara za uhakika katika maeneo yenye uwekezaji Mkubwa.
Ili kutokomeza kabisa vikwazo vya uzalishaji unaokidhi matakwa ya soko la kimataifa wakulima hao pia wameita serikali kupitia mamlaka ya udhibiti wa mbegu nchini TOSC kudhibiti uzalishaji holela wa miche ya parachichi isiyo na ubora ambayo inawatia hasara wakulima na kisha kuitaka kuweka ruzuku katika dawa,miche na huduma zote muhimu zinaztumika kuendesha kilimo hicho kwakuwa kinachangia pato kubwa
Wakizungumza na katika mkutano mkuu Avocado Society Tanzania (ASTA ) wakulima wa parachichi akiwemo Frank Msuya mkulima alishinda tuzo ya mkulima bora Kitaifa katika sherehe za Nane 2023 wamesema kwakuwa zao hilo linaingiz fedha nyingi za kigeni kama ilivyo kwenye Korosho ni vyema serikali ikaboresha miundombinu muhimu katika maeneo yenye uwekezaji mkubwa ili kuzalisha malighafi bora zinazokidhi matakwa ya soko la kimataifa.
Mambo hayo yanamuibua mwakilishi wa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Thadei Luoga ambaye anasema ni kweli zao hilo limekuwa liipa fedha nyingi za mapato halmashauri hiyo na kisha kudai kwamba ili kuhakikisha kilimo hicho kinashika kazi kwa kuzalisha malighafi bora wamenunua kifaa cha kupima ukomavu wa tunda na kisha kuweka bayana mwongozo mpya wa kilimo cha parachichi na masoko nchini ambao utasaidia kumpa tija mkulima .
Aidha Luoga amesema kwamba ili kudhibidi wanunuzi wanaonyonya wakulima katika halmashauri hiyo wamepiga marufuku makampuni kununua malighafi ya parachichi bila kupata kibali cha serikali hatua ambayo itasaidia pia kudhibiti uuzaji wa matunda ambayo hayaja komaa na kuharibu soko la Tanzania kimataifa.
Awali Dr Ibrahim Msuya ambaye ni Mkurugenzi ARM CITY CONSULTANTS akieleza kuhusu mradi mkubwa unaoenda kutekelezwa na serikali katika kijiji cha Ikang’asi kilichopo halmashauri ya wilaya ya Njombe amesema mkoa wa Njombe unakwenda kutekeleza kilimo cha Block Farming cha Parachichi katika eneo lenye ukubwa wa ekari elfu 80 ambapo huduma zote muhimu zitakuwa zikipatikana katika eneo hilo ili kuzalisha parachichi bora
Dr Msuya anasema katika kijiji hicho cha Parachichi katika ramani ya mradi serikali imetenga eneo la viwanda,mabwawa,Vitalu vya Miche,Zuu za Mifugo,Viwanja vya michezo,Nyumba za kuishi Utalaamu na huduma nyingine nyingi ambazo zitakwenda kufanya mageuzi ya kilimo hicho lulu sokoni kwasasa.
Kwa upande wao wanunuzi akiwemo Najib Kamrmali mkurugenzi wa kampuni ya AvoAfrica iliyojipambanua katika ununuzi wa malighafi ya parachichi wametumia mkutano huo kuwakumbusha wakulima kuhakikisha wanazingatia miongozo ya kilimo bora cha parachichi ikiwa ni pamoja na kuacha matumizi ya mbolea za chumvichumvi ambazo zinasababisha kuua soko la ughaibuni.
Najib amesema wakulima wamekuwa wakitaka bei nzuri kila siku lakini wana sahau kwamba ili upate soko la uhakika lazima kuzalisha malighafi inayohitajika sokoni.
Baada ya kupokea changamoto za kilimo cha parachichi,Ushauri na mapendekezo juu ya nini kifanyika ili kufanya mapinduzi katika kilimo hicho ndipo Rebeca Hepelwa Mwenyekiti ASTA akasema ili kurejesha ubora wa parachichi la Njombe ambao lilikuwa nao miaka yote ni kurudi kwenye msimu uliyozoeleka wa mavuno badala ya kuwahi kuvuna na kisha kutoa rai kwa wakulima kutotumia chumvichumvi ili kulinda soko.
“Ukitazama miaka michache iliyopita Parachichi ya Rungwe ilipoteza ubora huku Njombe ikionekana kuwa bora zaidi jambo ambalo limekuwa tofauti kwasasa kwasababu wakulima wa eneo hilo walirudi kujitathimini na kisha kuanza kuzingatia misingi ya kilimo hicho ili kupata malighafi Bora,alisema Rebecca Hepelwa mwenyekiti wa ASTA”
Kuhusu changamoto zilizosababisha Ubora wa parachichi ya Njombe kushuka Rebecca anasema wamezipokea changamoto zote na kisha kwenda kuzifanyia kazi ili kurejesha tena imani kwa wanunuzi juu ya ubora wa malighafi ya Njombe.