Afisa program jinsi,wanawake,vijana na watoto wa FDH,akikabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wasichana wa shule ya msingi Buigiri wasioona kuhusu uhumuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike
………………
Ofisa program Jinsia, Wanawake,Vijana na Watoto wa shirika wa shirika linalojihusisha na masuala ya kuhudumia watu wenye ulemavu la Foundation For Disabilities Hope (FDH) Halima Msofe, amesema jamii inapaswa kushirikiana kwa pamoja kutatua kero mbalimbali wanazokumbana nazo watoto wa kike hasa wenye ulemavu.
“Jamii inapaswa kushirikiana kwa pamoja kutatua changamoto za watoto wa kike na kuwapa msaada wanapohitaji lakini pia watoto wa kike wanaowajibu wa kujitambua na kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto zao”alisema Msofe
Msofe alibainisha hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa misaada ya vitu mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu wa shule ya Msingi Buigiri wasioona iliyopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike duniani.
Alisema jamii inalojukumu kubwa la kuwalinda watoto wa kike hasa wakati huu ambao kumekuwepo na wimbi kubwa na vitendo vya mmomonyoko wa maadili.
Pia aliwashauri mabinti kuripoti vitendo vya ukatili wa kijinsia kila wanapo kutana na hali hiyo iwe nyumbani au shule.
Aidha alisema misaada waliyotoa kwa watoto hao ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike duniani.
“Msaada tulitoa leo ni pamoja na taulo za kike, sukari, sabuni, pamoja na karamu”alisema Msofe
Afisa program jinsi,wanawake,vijana na watoto wa FDH akizungumza na wanafunzi wasichana wa shule ya msingi Buigiri wasioona kuhusu uhumuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike
Afisa program jinsi,wanawake,vijana na watoto wa FDH,akikabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wasichana wa shule ya msingi Buigiri wasioona kuhusu uhumuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike