Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo, Akizungumza na Viongozi na Wanachama wa (UWT) alipowasili Ofisi za Makao Makuu ya UWT leo Oktoba 12,2023 Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT),Jokate Mwegelo ameahidi kuwa muadilifu,mtiifu na kusema ameanza kazi rasmi ya kuhakikisha jumuiya hiyo inakuwa kimbilio na kivutio cha wanawake nchini.
Jokate ametoa ahadi hiyo leo Oktoba 12,2023 Jijini Dodoma baada ya kupokelewa na wanawake kwenye Makao Makuu ya Jumuiya hiyo.
Amesema kuwa ameanza kazi rasmi ya kuhakikisha jumuiya hiyo inakuwa na umoja na ushirikiano pamoja na kuwaunganisha wanawake wote watanzania ili wajue UWT ndio kimbilio lao la kwanza.
“Naendelea kumuomba anipe akili ya kukitumikia hiki kiti cha Katibu mkuu, Mwenyekiti wa CCM Rais Samia ameonesha imani kwa kundi kubwa la vijana pia ameonesha imani kuwa kwa wanawake wa kitanzania,”amesema Jokate
“Niwahakikishie nitafanya kazi kwa uadilifu, utiifu mkubwa sana, imani ambayo nimekopwa nitailipa kwa Imani, najua kuna mipango kazi, mikakati imewekwa mimi nipo tayari kupokea maelekezo yako Mwenyekiti wangu kwa jinsi ambavyo unatamani hii jumuiya iende nitachapa kazi pamoja na wewe mwendo wako si wa mchezo.”
Aidha amewahimiza kushikamana, kupendana na kushirikiana ili kuonesha uhalisia nguvu ya wanawake wa kitanzania.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda,amewaasa wanawake kushirikiana pamoja katika kuhakikisha wanatafuta ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.
Awali Katibu Mkuu Mstaafu wa UWT, Dkt. Philis Nyimbi, ameshukuru kwa nafasi aliyopewa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia kutumikia nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka miwili na kwamba ujio wa Jokate utaongeza kasi ya mafaniko ya jumuiya hiyo.
Oktoba Mosi mwaka huu Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM ilimteua Jokate Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa UWT akipokea kijiti kutoka kwa Dkt. Philis Nyimbi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo akipeana Mkono na Bi Asha Iddi alipokwenda katika Soko la Machanga leo Oktoba 12,2023 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo akilakiwa na Wanachama na Viongozi wa UWT alipowasili Ofisi za Makao Makuu ya UWT leo Oktoba 12,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo akifurahi Jambo Katika tukio la Mapokezi yake lililofanyika Makao Makuu ya (UWT) leo Oktoba 12,2023 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo, akifurahi na Kucheza na kulakiwa na Wanachama na Viongozi wa UWT alipowasili Ofisi za Makao Makuu ya UWT Dodoma.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg.Jokate Mwegelo, Akizungumza na Viongozi na Wanachama wa (UWT) alipowasili Ofisi za Makao Makuu ya UWT leo Oktoba 12,2023 Dodoma.