Muhitimu wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Alvine Antony aliyebuni teknologia itakayozuia ajali kati ya treni na vyombo vya moto.
Hiyo ndio teknologia bunifu itakayozuia ajali kati ya treni na vyombo vya moto ikiwemo magari na pikipiki ambazo zimekuwa zikitokea katika makutano ya njia za reli na barabara.
Muhitimu wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Alvine Antony akiwa ameshita romoti kwa kuendelea na teknologia hiyo bora nchini
Afisa uhusiano wa NIT Juma Manday akisisitiza jambo juu ya teknologia ambaye anasema itakuwa mwarubani wa kwa kuzuia ajli kwenye makutano ya barabara na reli
Na Lucas Raphael,Tabora
Muhitimu wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Alvine Antony amebuni teknologia itakayozuia ajali kati ya treni na vyombo vya moto ikiwemo magari na pikipiki ambazo zimekuwa zikitokea katika makutano ya njia za reli na barabara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati akielezea mfumo huo katika maonesho ya maadhimisho ya usalama wa reli ambayo yanafanyika kitaifa mkoani Tabora .
Alisema kwamba mfumo huo ameuunda ukiwa na uwezo wa kutambua ikiwa treni inapokaribia makutano ya barabara na reli taa za barabarani ziwawaka kuzuia magari, na mageti yanafunga pande zote na kuruhusu treni kupita na badaye milango hiyo kufunguka ili kuruhusu vyombo vya moto kupita na watembea kwa miguu baada ya treni kupita eneo la makutano.
Alvine alisema kwamba amefanya ubunifu huo kwa muda wa mwezi mmoja wakati wa masomo yake katika chuo hicho.
Hata hivyo aliiomba serikali na wadau wa usafiri wa reli kumshika mkono katika kuboresha bunifu hiyo ili kupunguza ajali katika makutano ya reli na barabara.
Aidha alisema kuwa teknolojia hiyo inaweza kutumika katika kusaidia kuondokana na wimbi la ajali ambazo zimekuwa zikitokea katika makutano ya njia za reli na barabara nchini
Afisa uhusiano wa NIT Juma Manday alisema kwamba teknologia hiyo ndio itakuwa mwarubaini wa kupunguza kutokea kwa ajali kwenye makutano hayo.
Alisema maeneo hayo yamekubwa na matukio ya ajali za mara kwa mara lakini uwepo wa teknologia hiyo kutoka katika chuo cha Taifa cha Usafirishaji itasaidia kwa asilimia kubwa kupunguza ajali hizo.
Alitoa wito kwa wadau mbalimbali watembelee banda la chuo cha Taifa cha usafirishaji ili kupata maelezo ya kozi mbalimbali znazotolewa na chuo hicho.