Wamesema usalama wao upo pabaya kwasababu kuna biashara kubwa zinafanyika katika soko hilo zikihusisha mabilioni ya fedha na wateja kutoka nchi za Rwanda,Malawi Burundi Uganda Congo Zambia na Msumbiji hivyo ni vyema serikali ikaboresha huduma zote muhimu katika soko hilo ambalo linachangia Mapato mengi katika halmashauri ya mji Makambako.
Katika mkutano wenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ,Wafanyabiashara wa soko hilo akiwemo Bryson Kyando licha ya kufanya biashara kubwa za mazao na kuingiza mabilioni ya fedha lakini hakuna mtandao wa simu ,Barabara za uhakika maji ,Kituo cha polisi na taasisi za fedha na kisha kukiomba chama cha mapinduzi kufikisha kero hizo serikalini.
Kuhusu suala la Mtandao wa simu Kyando amesema mtandao wa simu hususani Internet ni muhimu kuwepo katika soko hilo kwasababu biashara za sasa zinafanyika kwa njia simu kwani wamekuwa wakituma picha za malighafi kwa wateja wao kuwa njia ya Whatsupp hivyo wanaomba serikali kujenga mnara au kuongeza nguvu za minara ya karibu ili kuongeza ufanisi kibiashara.
“Kwa kuwa halmashauri inapata mapato tuombe uboreshaji wa barabara za ndani ya soko na nje ya soko ,kituo cha polisi kijengwe hapa na taasisi za fedhakama mabenki yaje hapa ili kuweka usalama wa fedha za wafanyabiashara na wateja wanaokuja na mamilioni ya fedha kununua mazao,alisema Bryson Kyando makamu mwenyekiti wa vizimba soko la Makatani Lyamkena”
Akitoa ufafanuzi juu ya hatua za kuwasaidia wafanyabiashara wa soko hilo la mazao baada ya kupokea kero zao na Mipango ya halmashauri ya mji Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe ambaye ni Mbunge wa Makambako Deo Sanga anasema kwa kuwa soko hilo la kimataifa limetengeneza ajira nyingi za watu anakwenda kusaidia ujenzi wa kituo cha polisi kwa kujenga msingi na kisha kuiomba serikali kumalizia.
Aidha Sanga amesema changamoto ya mawasiliano ya simu alikuwa akiitambua na tayari imewasilishwa wizarani ambako minara zaidi ya 700 imetengwa kwa ajili kuboresha mawasiliano kote nchi huku akisema kwa eneo hilo serikali italifanyia tathimini ya kina ili kujua kama panahitaji mnara ama kuongeza nguvu ya mtandao kwa minara ya jirani.
Katika Hatua nyingine amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Makambako Kuhakikisha anatenga eneo la kujenga kituo kidogo cha polisiili aanze ujenzi wa msingi huku meneja wa Tarura na tanroads akiwataka kumaliza adha ya miundombinu ya barabara na vivuko kuelekea sokoni hapo.
“Eneo la soko linahitaji kuwa na mawasiliano ya simu ya uhakika hivyo tunakwenda kulifanyia kazi tatizo hilo ,alisema Deo Sanga mwenyekiti wa CCM Njombe
Baada ya mwenyekiti wa CCM kueleza msimamo wake wa kuhakikisha miundombinu inaboreshwa katika soko hilo la mazao ndipo meneja wa TARURA Njombe Mhandisi Gerard Matindi na mwakilishi wa meneja wa TANROARDS Njombe Nhandisi Aloyce Matete wakaweka bayana wanachokwenda wanachokwenda kufanya ikiwa ni pamoja na kutuma wahandisi kuja kuchunguza eneo la ujenzi.