NJOMBE
Wananchi wa Kijiji Cha Luponde kilichopo Halmashauri ya mji wa Njombe ambacho kimezungukwa na wawekezaji na kikicho Cha chai na kituo Cha utafiti wa mazao Cha IGELI wameomba serikali kuwasaidia kupata ardhi Yao ya kilimo WALIYOKUWA wakulima vizazi na vizazi ambayo imepokwa na kituo Cha Utafiti.
Wananchi Hawa wanasema wako kwenye hatari ya kukumbwa na baa la njaa kwasababu katika Kijiji chao hawana ardhi ya kufanya shughuli za uzalishaji wa mazao ya kilimo na kwamba hata ardhi ya Igeli waliyokuwa wakitumia kwa uzalishaji wa chakula limepokwa mwaka huu.
Wakizungumzia changamoto hiyo Mara baada ya mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi ccm(MNEC) Taifa Mkoa wa Njombe Daniel Okoka kukagua mradi wa kituo Cha afya Cha Luponde wakazi wa Luponde akiwemo Erasto Mwalongo wanasema wanashangazwa kuona serikali inawahamasisha kununua mbolea kwa ajili ya msimu mpya wa kilimo wakati wawekezaji wamepoka ardhi yote ya kilimo hivyo wanaomba chama na serikali kuona namna ya kuwasaidia kabla ya kukumbwa na njaa.
“Tunashukuru kutusaidia kupata huduma nyingine Kama afya na mbolea lakini tunaomba mtusaidie kupata ardhi ya kilimo Igeli kwasababu watu wameondolewa katika mashamba waliyokuwa wakulima kipindi chote kwa madai ya kupisha muwekezaji wa kituo Cha Utafiti ,alisema Erasto Mwalongo mkazi wa Luponde”
Fridolini Mwalongo ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Luponde amekiri kuwepo kwa changamoto ya ardhi na Kisha kueleza athari kubwa iliyopo kwasasa kijijini hapo kutokana na kukosa ardhi ya kilimo huku kueleza shida ya maji.
“Hilo eneo la Igeli tulipewa eneo la chini kulima mazao wananchi lakini tunashangaa Sasa muwekezaji amezuia na Kuweka bikoni hivyo tuko kwenye hatari ya njaa,alisema Fridolini Mwalongo Mwenyekiti wa Kijiji Cha Luponde”
Akitoa ufafanuzi juu ya hatua wanazokwenda kuchukua ili kumaliza changamoto hiyo mjumbe wa halmashauri kuu taifa ya chama cha mapinduzi Mkoa wa Njombe Danieli Okoka anasema wamepokea Kero hiyo na kuiwasilisha katika kikao Cha majumuisho mnamo octoba 6 na Kisha kutolea maamuzi ili kunusuru Maisha ya watu wa Luponde .
Amesema Wanakwenda kuunda time itakayochunguza haki za watu na muwekezaji na Kisha kuirudisha majibu .
Awali katibu siasa na uenezi wa chama Cha mapinduzi mkoa wa Njombe Josaya Luoga amezungumzia changamoto ya maji kwa wakazi wa Luponde na Kisha kuahidi kwamba serikali inatekeleza mradi mkubwa wa maji utakaonufaisha Luvuyo na Luponde ambao baada ya miezi miwili utakuwa umekamilika .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Scolastica Kevela emetumia ziara hiyo kuongea na wazazi juu ya suala la malezi kwa watoto hususani katika maadili huku pia akiwataka kutovuka MIPAKA Yao
Aidha Scolastica amesema kwakuwa CCM ndiyo yenye ilani inayotekelezwa Sasa hivyo wanapita kukagua miradi ya maendeleo ambayo unaotekelezwa baada ya Rais kutoa mabilioni ya fedha kwa wakazi wa Njombe
“Niwaombe wazazi Kuzingatia maadili na malezi ya watoto wetu kwasababu kumekuwa na changamoto kubwa kwasasa ,alisema Mwenyekiti wa UWT Njombe Scolastica Kevela”
Katika ziara hiyo kamati imetembelea na kukagua miradi mingine ukiwemo wa bweni na nyumba ya mwalimu sekondari ya Matola na jengo la ghorofa sekondari ya Uwemba.