Mhandisi Isaya Mosha akifafanua jambo kwa Naibu Waziri waUjenzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabora- Kigoma sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 99.
Na Lucas Raphael, Tabora
Naibu Waziri wa Ujenzi mhandisi. Godfrey Kasekenya amesema kwamba wizara inafanya jitiada kuhakikisha kilomita 51.1 zilizobaki zinamalizika haraka ili kuweza kuunganisha mkoa wa Tabora na Kigoma kwa kiwango cha lami .
Aliotoa kauli hiyo alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabora- Kigoma sehemu ya Kazilambwa-Chagu kwa upande wa Tabora yenye urefu wa KM 36 na Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1upande wa kigoma.
Alisema kwamba kukamilika kwa barabara hiyo kwa kiwango cha lami kutachochea maendelea kwa kasi na kukuza uchumi wa wananchi wa mikoa ya mbalimbali nchini.
“Kwa kweli nimeridhika na kasi ya ujenzi sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 kwa kwango cha lami ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 99”,alisema mhandisi Kasekenya.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo amemtaka mkandarasi STECOL Cooperation Ltd anayejenga sehemu ya Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1 kufanya kazi
usiku na mchana ili kuandika historia ya kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa kiwango cha lami mapema iwezekanavyo.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Mhandisi Narcis Choma alisema ujenzi huo umefikia asilimia 45 na watamsimamia
kikamilifu mkandarasi ili maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua yakamilishwe mapema ili kuepuka visingizio na kuwawezesha wasafiri na
wasafirishaji wa mikoa hiyo kunufaika na barabara ya kisasa.
Alisema kwamba kiasi cha shilingi bilioni 62.7 zinatumika katika ujenzi huo ambazo ni matapo ya ndani na mkopo nafuu kutoka mifuko ya OPEC na Abu Dhabi.
Awali Naibu Waziri Kasekenya alimtaka Mkandarasi Beijing Construction Engineering Group (BECG), anayejenga jengo kupumzikia abiria na mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Tabora kuongeza kasi ya ujenzi kwani Serikali imedhamiria kuufungua ukanda wa Magharibi mwa Tanzania kwa miundombinu yote ya ardhini, majini na angani ili kuwawezesha wawekezaji na wazalishaji kuibua fursa zilizoko katika ukanda huo na hivyo kukuza uchumi wa nchi.
Naibu Waziri huyo wa Ujenzi yuko katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Rukwa na Katavi.