Na Ashrack Miraji
Mkurugezi wa Tasisi ya Fahari Tuamke maendeleo. Bi Neema Willgard Mchau ametoa msaada wa mahitaji muhimu wenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili na Laki Saba kwa wanafunzi viziwi katika Shule ya Msingi mzambarauni Mkoani Dar es salaam kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika program ya ‘Tabasam na Mama’
Bi Neema amesema ametoa msaada huo kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa anaguswa na matatizo mbalimbali ya watoto wenye uhitaji hapa nchini kwa kuwachangia gharama za matibabu na kuwapatia misaada mbalimbali.
“Fahari Tuamke maendeleo tumeamua kuendeleza program ya Tabasam na Mama kwa kuchangia mahitaji muhimu kwa wenye uhitaji na program hii kwetu itakuwa endelevu”amesema Bi.Neema
Mbali na hayo pia ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ofisi na Mkurugezi wa Almashauri pamoja na Ofisi ya Afisa mtendaji wa kata hiyo kwa kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kuwafikia watu wenye uhitaji.
Aidha Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wakina mama kuwa mstari wa mbele katika kumuunga mkono Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya.
Mkuu wa shule ya Msingi Mzambarauni kingengo Maalum George Njau amemshukuru kwa msaada aliotoa kwa watoto hao na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano kwa kuwasaidia watoto wenye uhitaji.