Na John Walter-Manyara
Serikali imetoa shilingi Bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Wasichana ya mkoa wa Manyara, inayojengwa katika Kijiji cha Kiongozi kata ya Maisaka wilaya ya Babati.
Akzingumza na wazee, viongozi wa dini na mila mjini Babati katika kikao maalum,mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari imetoa fedha za kujenga Shule mpya maalum ya Sekondari ya Bweni na sayansi kwa ajili ya wanafunzi wa kike na kwamba ujenzi umeanza kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Serikali ilitenga Shilingi Trilioni 1.2 kwa ajili ya kujenga shule mpya za Sekondari 1,026 nchi nzima zikiwemo shule 26 Maalum za wasichana zinazojengwa moja kila mkoa.
“Katika kipindi alichopo madarakani rais wetu mpendwa Dr Samia Suluhu Hassan katika mkoa wetu pekee ametupatia fedha za maendeleo shilingi bilioni 498” alisema Sendiga