Mtendaji Mkuu wa Benki ya Letshego Faidika Bank, Bw Baraka Munisi (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao. Kushoto ni meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika bw Asupya Nalingigwa. Kampeni ya Kopa Tukubusti ina lengo la kuwafaidisha wateja wao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha taslimu. Kupitia kampeni hiyo, mteja anaweza kushinda hadi asilimia 50 ya fedha alizokopa katika benki hiyo.
Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Joram Mtafya (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kopa Tukubusti ya benki ya Letshego Faidika. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Leshego Faidika, Baraka Munsi. Kampeni ya Kopa Tukubusti ina lengo la kuwafaidisha wateja wao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha taslimu. Kupitia kampeni hiyo, mteja anaweza kushinda hadi asilimia 50 ya fedha alizokopa katika benki hiyo.
Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Joram Mtafya (katikati) akipozi mara baada ya kuzindua rasmi kampeni ya Kopa Tukubusti ya benki ya Letshego Faidika. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Leshego Faidika, Baraka Munisi na kulia ni Afisa Masoko wa benki hiyo, Hindu Juma.Kampeni ya Kopa Tukubusti ina lengo la kuwafaidisha wateja wao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha taslimu. Kupitia kampeni hiyo, mteja anaweza kushinda hadi asilimia 50 ya fedha alizokopa katika benki hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Letshego Faidika, Baraka Munisi (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Ukaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Joram Mtafya (wa pili kulia) na maofisa mbalimbali wa benki hiyo na wa kampuni ya maarufu ya kuandaa matukio mbalimbali na masoko, Radian Limited chini ya Afisa mtendaji Mkuu Freddie Manento (wa kwanza kulia). Kampeni ya Kopa Tukubusti ina lengo la kuwafaidisha wateja wao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha taslimu. Kupitia kampeni hiyo, mteja anaweza kushinda hadi asilimia 50 ya fedha alizokopa katika benki hiyo.
Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam.
Benki ya Letshego Faidika imezindua kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la KOPA TUKUBUSTI yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao kwa kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha taslimu. Kupitia kampeni hiyo, mteja anaweza kushinda hadi asilimia 50 ya fedha alizokopa katika benki hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Letshego Faidika Bank, Bw Baraka Munisi alisema kuwa “lengo kubwa ya kampeni hiyo ni kuwafaidisha wateja wao. Alisema kuwa ubunifu walioufanya utawawezesha kuinua vipato vya wateja na kumudu gharama mbalimbali za maisha.”
Bw Baraka Munisi alisema kuwa “benki yao inawajali wateja wao na kuamua kuanzisha kampeni hiyo itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu (siku 90).”
Kwa upande wake, meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika bw Asupya Nalingigwa alifafanua kuwa watakuwa wanafanya droo ya kutafuta washindi kila baada ya wiki mbili ambapo jumla ya washindi 30 watazawadiwa zawadi mbalimbali.
“Kampeni hii ina lengo la kuwawezesha au kuwafaidisha wateja wetu, ambapo zawadi ya kwanza ni kiwango cha fedha cha asilimia 50 ya fedha ya mkopo ambapo mteja wetu alikopa. Pia tutakuwa na zawadi nyingie za fedha taslimu, pikipiki, fulana na shajara (Diary),” alisema Asupya Nalingigwa.
Kwa mujibu wa Bw Nalingigwa, vigezo mbalimbali vimewekwa kwa washiriki wa kampeni hii ikiwa pamoja na umri kuanzia miaka 18, lazima awe mfanyakazi aliyethibitishwa wa serikali na taasisi binafsi na lazima awe na sifa za kupata mkopo kwa mujibu wa vigezo na masharti.
“Pia mteja ambaye ataingia kwenye kampeni hii lazima ajaze fomu maalum ya kukubali vigezo na masharti yaliyowekwa. Tunawaomba wateja wetu kushiriki kwa wingi katika kampeni hii yenye lengo la kuwafaidisha. Benki yetu inawajali wateja wake na kuanzisha kampeni hii kwa ajili yao,” alisisitiza Bw Asupya Nalingigwa.
Benki ya Letshego Faidika ni muunganiko wa taasisi mbili za kifedha za Letshego Tanzania na Faidika na ilianza rasmi shughuli za kibenki mwezi Julai mwaka huu (2023).