Na. Damian Kunambi, Njombe.
Wakazi zaidi ya 40,000 wa Tarafa ya Liganga wilayani Ludewa mkoani Njombe wameondokana na adha ya kutbea umbali wa zaidi ya km. 50 kufuata huduma ya afya baada ya serikali kutoa fedha kiasi cha sh. Mil 500 ambazo zimewezesha kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kwa asilimia 100 ulio ambatana na unujuzi wa vifaa Tiba vyenye thamani ya sh. Mil 150.
Kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho iliyowasilishwa mbele ya mkuu wa wilaya ya Ludewa Bi. Victoria Mwanziva wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo hicho imeeleza kuwa kituo hicho kilianza ujenzi wake kwa nguvu za wananchi kwa kuchangia kiasi cha zaidi ya sh. Mil 41 huku wahisani wakichangia kiasi cha sh. Mil. 2.5 ndipo serikali ikaleta kiasi hicho cha fedha kilichowezesha kukamilisha ujenzi huo.
Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Sunday Deogratius amesema katika kuhakikisha wananchi hao wanapata huduma iliyo bora Halmashauri hiyo kupitia bajeti ya mwaka 2022/2023 ilitenga fedha kiasi cha sh. Mil 150 kwaajili ya ununuzi wa vifaa Tiba na dawa ambavyo navyo vimezinduliwa sambamba na kituo hicho.
Deogratius amesema pamoja na ununuzi wa vifaa hivyo lakini bado kuna uhitaji wa vifaa vingine zaidi ambapo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea fedha za maendeleo ya Halmashauri hiyo kwa mwaka 2023/2024 kiasi cha sh. Bil. 1.5 katika muda muafaka ambapo kupitia fedha hizo Halmashauri hiyo itaenda kutenga tena kiasi cha sh. Mil. 150 ili ziweze kuongeza vifaa zaidi vya kituo hicho.
Hata hivyo kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Wise Mgina amwishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuunga mkono juhudi za wananchi huku akiwasilisha ombi la kukipandisha hadhi kituo hicho cha afya na kukifanya kuwa Hospitali kwani katika siku zijazo kata hiyo itakuwa na muingiliano mkubwa wa watu pindi mradi mkubwa wa Liganga utakapoanza kufanya kazi.
Alatukolela Kihombo ni miongoni mwa wananchi hao amesema kuwa wamekuwa Kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho iliyowasilishwa kwa mkuu huyo wa wilaya katika hafla ya uzinduzi huo imeeleza kuwa kituo hicho cha afya kinaenda kunufaisha wakazi zaidi ya elfu arobaini wa Tarafa ya Liganga ambao hapo awali walikuwa wakikumbwa na changamoto juu ya upatikanaji wa huduma hiyo.
Naye mganga mkuu wa Wilaya hiyo Stanley Mlaya amesema kituo hicho kinaenda kutoa huduma ya wagonjwa wa nje,chanjo, uzazi, vipimo vya maabara,uteketezaji wa taka, huduma ya upasuaji kwa akina mama wajawazito na wagonjwa wengineo.
“Napenda niwasihi wagonjwa mbalimbali kujitokeza kuja kupata huduma katika kituo hiki na hasa akina mama wajawazito kwani huduma zao hutolewa bure ukizingatia tayari kuna vifaa tiba vya kutosha kwaajili ya kuhudumia wagonjwa watakao jotokeza”. Amesema Mlay.
Akizindua kituo hicho mkuu wa wilaya Victoria Mwanziva amesema katika kipindi hiki cha uongozi wa serikali ya awamu ya sita suala la huduma ya afya imekuwa likipewa kipaumbele kwani wilaya ya Ludewa tayari imepokea fedha nyingi za kuboresha huduma hiyo ikiwemo kiasi cha sh. Mil 900 kwaajili ya kuboresha miundombinu ya majengo katika Hospitali ya wilya hiyo, Mil. 200 kwaajili ya kukamilisha zahanati ya Kitongoji cha Chimbo, zahanati ya Mkiu, Kimelembe ambazo zote tayari zimekamilika na kuanza kutoa huduma huku zahanati ya kijiji cha Ndowa ujenzi wake ukiendelea.
Kuhusu mapokezi ya vifaa tiba Mwanziva amewaagiza watoa huduma kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kutumika kwa muda mrefu huku akiyaomba mashirika mbalimbali pamoja na wadau wa afya kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya kwa kuleta vifaa tiba ili wananchi waweze kupata huduma iliyo bora zaidi na kuwaasa wananchi hao kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili waweze kupata huduma kwa gharama nafuu.
“Tunamshukuru mama yetu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mbunge wa jimbo la Ludewa kwa ushiririkiano wao uliowezesha kupatikana kwa fedha hizo za miradi kwani Rais huyo amekuwa akifika kusiko fikika kwa kuleta Fedha za kuboresha miundombinu hii ya afya na si hizo tuu bali hata katika miradi mingine kama ya elimu na barabara “, Amesema Bi. Mwanziva.