Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Yessir Mohd Juma akizungumza na Maofisa Tehama na Utumishi wa Sekta za Umma wakati akitoa taarifa ya hali ya usajili wa wafanyakazi katika Mfuko huo huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Maofisa Tehama na Utumishi wa Sekta za Umma wakifuatilia taarifa ya hali ya usajili wa wafanyakazi katika Mfuko wa Huduma za Afya huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Afisa Tehama Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Tawwakal Shams Khamis akiwaelekeza maafisa tehama na Utumishi wa Sekta za Umma juu ya hatua za kuchukua endapo mfanyakazi atakwama katika kujiunga na huduma ya ZHSF huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Ofisa Utumishi Halmashauri ya Manispaa ya Magharibi A Mafunda sadik Ali akiuliza suali kwa maofisa wa ZHSF wakati wakipatiwa taarifa ya hali ya usajili wa wafanyakazi katika Mfuko wa Huduma za Afya huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Ofisa Tehama Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Idarous Saleh Said akiuliza suali kwa maofisa wa ZHSF wakati wakipatiwa taarifa ya hali ya usajili wa wafanyakazi katika Mfuko wa Huduma za Afya huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
Mkuu wa Divisheni ya utawala Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Abdulla Mohammed Haji akiuliza suali kwa maofisa wa ZHSF wakati wakipatiwa taarifa ya hali ya usajili wa wafanyakazi katika Mfuko wa Huduma za Afya huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.
PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO
Na Rahma Khamis Maelezo
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar Yassir Ameir Juma amewataka watoa huduma za Afya katika vituo vya Vikosi vya Ulinzi na usalama kubadilika kutoa huduma bora zaidi.
“Tutowe huduma kwa moyo safi kwa kufata miongozo ya afya ili tusije kuvutana katika safari yetu tunayotaka kuianza,” alisisitiza. Kaimu
Akifunga mafunzo ya kuwajengea uwelewa juu ya huduma bora kwa wananchi katika Ukumbi wa Michenzani Mall amesema wakati wanapotaka kutoa huduma bora kwa wananchi lazima kubadilika ili kuondoa malalamiko.
Aidha amewasihi watoa huduma hao wa kuimarisha huduma ya uhakika kwa moyo wa kujitolea ili kuepusha migogoro kati ya wananchi na watoa huna hizo.
Amesema lazima watoa huduma wawe wabunifu wa kubuni mbinu mbalimbali za kuwavutia wateja wao ikiwemo madakatari wao kujituma katika kazi, kuboresha majengo na kuwa na vifaa tiba vya kutosha.
“Wenzetu watoa huduma wa vituo binafsi wamejipanga kwa kila kitu kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wananchi vipi sisi tumejipanga je kuhusu hili,” aliuliza Kaimu Mkurugenzi huyo.’’
Nae Afisa Mdhibiti Ubora wa huduma za Afya Ahmed Saidi Moh’d amesema wanafanya mabadiliko ya sera ya afya kwa kuanzisha taasisi inayoshughulikia upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi wote na kua endelevu.
Amesema huduma za afya zilikuwepo tokea awali lakini zilikua hazina viwango hinyo wamedhamiria kuziboresha zaidi huduma hizo ili ziweze kupatikana kwa uhakika.
“Kuanzishwa kwa mfuko huu ni tija kwetu kwani tutakusanya fedha nyingi kulingana na kipato chetu, kupitia mfuko huu tutahakikisha zinakidhi kuhudumia wananchi wote wa Zanzibar” alisema.
Aidha amefahamisha kuwa kulingana na misingi ya kuanzishwa kwa mfumo huo wameweza kugawa makundi tofauti ya kusaidiana ikiwemo walemavu wagonjwa na waiojiweza.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameumba Mfuko huo kusaidia hospitali ambazo zina upungufu wa vifaa jambo ambalo litasaidia kuondosha usumbufu kwa wananchi.
Wamesema wakati watakapopelekewa mikataba katika hospitali zao wapatiwe na orodha ya hospitali ambazo zitatumia huduma hizo ili kuwaondeshea usumbufu wagonjwa.
Aidha wamefahamisha kuwa kupitia mafunzo hayo watahakikisha wanajiimarisha zaidi kwa kuweka vifaa vya kutosha ili kutoa huduma bora na kuitaka jamii kutumia fursa hiyo na kuacha kusikiliza maneno ya mitaani.
Mafunzo hayo ya kuwajengea uwelewa juu ya Mfuko wa Huduma za Afya ni ya siku tatu na yameandaliwa na Watendaji wa Mfuko huo na kuwashirikisha watoa huduma katika Taassisi za Umma na Binafsi