NAIBU Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk.Dotto Biteko,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango leo Septemba 6,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum; Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania uliofunguliwa na Naibu Waziri Mkuu Mhe Dk.Dotto Biteko, kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango leo Septemba 6,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati yakudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii,Mhe.Fatma Toufiq,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania ulioanza leo Septemba 6 hadi 7 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deogratius Ndejembi,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania ulioanza leo Septemba 6 hadi 7 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania ulioanza leo Septemba 6 hadi 7 jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobasi Katambi,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania ulioanza leo Septemba 6 hadi 7 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Dkt.Dotto Biteko (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania ulioanza leo Septemba 6 hadi 7 jijini Dodoma kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe.Dkt.Philip Mpango.
Wadau mbalimbali wakizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania uliofunguliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Dkt.Dotto Biteko kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe.Dkt.Philip Mpango ulioanza leo Septemba 6-7 jijinin Dodoma.
NAIBU Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk.Dotto Biteko,akiwa katika picha ya pamoja na watoto mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii Tanzania kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango leo Septemba 6,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk.Dotto Biteko ametoa maelekezo mahsusi kwa Ofisi ya Rais, Tamisemi na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum.
Dkt.Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati ametoa maelekezo hayo leo Septemba 6,2023 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa Maofisa Ustawi wa Jamii Tanzania kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango.
Dkt.Biteko ameitaka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Ofisi ya Rais TAMISEMI na wadau wengine ikiwemo ya kuhakikisha kuwa mchakato wa mapitio ya sheria ya mtoto na kanuni zake unakamilika ili kuhakikisha watoto wanapata ulinzi na malezi stahiki.
”Hakikisheni mchakato sheria ya wataalamu wa ustawi wa jamii inakamilika ili kupanua wigo na kusimamia maadili wa utoaji wa huduma za ustawi wa jamii.”amesema Dkt.Biteko
Aidha, Wakurugenzi wa Halmashauri wametakiwa kutenga fedha kwa ajili ya huduma za Ustawi wa Jamii kwa mujibu wa mwongozo wa mipango, bajeti na taarifa za Ustawi wa Jamii.
Vilevile, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wametakiwa kuendelea kutoa ajira kwa maafisa Ustawi wa Jamii ili kusaidia kutoa huduma bora za Ustawi wa Jamii
Dkt. Biteko ameagiza pia kuimarishwa kwa programu ya huduma ya afya ya akili na msaada wa kisaikolojia ili kupunguza athari na changamoto zinazotokea ndani ya familia na jamii.
Agizo jingine lililotolewa ni uwekaji wa mfumo madhubuti wa ufuatiliaji wa makao ya Watoto na Makazi ya wazee ili kuhakikisha malengo ya msingi ya kuanzishwa vituo hivyo yanafuatwa kikamilifu na hayaanzishwi kiholela;
Aidha, Wizara ya Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta pamoja na Wadau wa Maendeleo imetakiwa kufanya tafiti ili kupata taarifa sahihi na takwimu ili kuboresha huduma za Ustawi wa Jamii.
Pia, Wizara ya Afya imeagizwa kuunda kitengo Maalum kitakachoshughulikia uratibu wa huduma za ustawi wa Jamii kutokana na umuhimu wa wataalamu wa Ustawi wa Jamii katika huduma za afya.
Dkt.Biteko amesema, Serikali imeendelea kuipa kipaumbele sekta hiyo kwakuwa imekuwa kimbilio la wananchi wenye uhitaji wa huduma hiyo na kuwahakikishia kutoa ushirikiano muda wowote.
Aidha,amesema sekta ya ustawi wa jamii ikifanya kazi kwa weledi na ufanisi itapunguza mzigo kwa Serikali kwa kuwa changamoto za kijamii zitapungua na fedha ambazo zimetengwa zitatumika katika kuendeleza maendeleo mengine.
Awali Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum; Dkt. Dorothy Gwajima, amewataka watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili huduma hiyo ya ustawi wa jamii iwafikie wananchi wote ambao wanahitaji, pia amewapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya..