MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kutembelea Banda la Benki ya Posta kwenye maonyesho ya saba ya
biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini
Tanga kulia ni MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne
Wagana na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi
Zena Said
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Edward Bukombe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la TPB Benki kushoto ni MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana |
MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana aliyevaa koti jeusi akizungumza na wageni mbalimbali waliotembelea banda lao kwenye maonyesho hayo |
MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana kulia
akisalimiana na kiongozi wa TCCIA Mkoani Tanga wakati wa maonyesho hayo
Maafisa wa Benki ya Posta Tawi la Tanga (TPB) kulia
wakimsikiliza mmoja wa wakazi wa Jiji la Tanga aliyetembelea Banda
lao
MENEJA wa Tawi la Benki ya TPB la Tanga Jumanne Wagana kushoto
akimkabidhi zawadi kiongozi wa TCCIA ambao ndio waandaaji wa maonyesho
hayo
WAJASIRIAMALI wadogo na wa kati wapatao 3400 mkoani Tanga wamenufaika na
mikopo kutoka Benki ya Posta (TPB) wenye thamani ya Bilioni 9.1 ambao
umewawezesha kujikwamua kiuchumi.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Benki ya Posta (TPB) tawi la Tanga Jumanne
Wagana wakati wa maonyesho ya Biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye
viwanja vya Mwahako Jijini hapa.
Alisema kwamba mikopo hiyo ilitolewa pia kwenye vikundi mbalimbali,
watumishi wa umma na wazee waastaafu kwa mkoa mzima wa Tanga.
Aidha alisema wakati wanaanza kutoa mikopo hiyo mwaka jana waliweza
kuitoa kwa wateja 3000 ambao ulikuwa na thamani ya sh.bilioni 8 huku
wakiweka lengo la kuwafikia wateja wengi zaidi.
Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo ni baadhi ya wateja kushindwa
kurudisha mikopo hiyo kwa wakati huku wengine wakiwa na mikopo zaidi ya
mmoja.
Hata hivyo aliwataka wateja wao kuendelea kutumia huduma zao mara kwa
mara kwa sababu mikopo yao wanatoa kwa riba nafuu na huduma nzuri
zinazowajali wateja wao.
Naye kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ambaye
alitembelea banda hilo aliipongeza Benki hiyo kwa kuwawezesha wakazi
wa mkoa huo kunufaika na mikopo ambayo imekuwa mkombozi kwao.
Alisema kwamba mikopo hiyo inasaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea
wafanyabiashara na wajasiriamali kukuza kipato chao na hivyo kupata
mafanikio .