Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amekagua mradi wa ulazaji Bomba la Gesi asilia kutoka kitalu cha Ntorya hadi kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba, mkoani Mtwara, akiwa ziarani mkoani humo, leo tarehe 13 Novemba 2026. 

Mradi huo unaogharimu takribani Sh bilioni 119. Ulazaji wa bomba umekamilika, huku uunganishaji wa mwisho ukiendelea. 

Bomba hilo lenye urefu wa takriban kilomita 34 litasafirisha gesi asilia kutoka Ntorya hadi Madimba, na kuongeza upatikanaji wa gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme na matumizi ya viwandani, usafiri pamoja na matumizi ya majumbani kama kupikia. 

Akiwa katika eneo hilo, Makamu wa Rais, ameridhishwa na utakelezaji wa mradi huo ambao utachochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi wa Mtwara na Taifa kwa ujumla.