Na Ahmed Mahmoud
IMEELEZWA kwamba Teknolojia haizifanyi huduma za Posta duniani kupitwa na wakati Bali zinafanya huduma ziwe za kisasa zaidi kuendana na matumizi ya Teknolojia mpya za kigitali na gharama nafuu.
Aidha RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuzindua Jengo la Umoja wa Posta barani Afrika Tarehe 2 mwzi ujao akiambatana na Marais watano Kutoka mataifa ya Afrika.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Selestine Kakele wakati akifungua Mkutano wa 41 wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika PAPU Jijini Arusha kaskazini Mwa Tanzania.
Amesema kwamba Shirika la Posta nchini wanayo nafasi kubwa ya kuendesha shughuli zao kutokana na kuwa na miundombinu kila eneo hii inasaidia kutumia Teknolojia za kibiashara za mtandao kuwafikia wateja wao (e comance).
“Kikao nilichufungua Leo ni sehemu ya Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika PAPU likiwa ni kikao Cha Ufundi Kwa siku mbili halafu wanachambua ripoti na kupeleka kwenye kikao Cha Baraza la Utawala Kwa ajili ya maamuzi”
Alisema kamati hizo za ufundi zinatakiwa kuja na mapendekezo na yanayopimika na yanaoyotekelezeka kufanya mashirika ya Posta barani Afrika yazidi kuonekana umuhimu wake kujiendesha Kwa ufanisi katika Dunia ya kidigitali.
Alisema mchango wa mashirika ya Posta katika kuhakikisha tunafanya vizuri ni mkubwa Sana kutokana na kwanza kuwa na miundombinu ya msingi Sana ikiwemo anuani za makazi kila mahali hapa nchini.
Alisema Teknolojia hazifanyi Shirika la Posta kupitwa na wakati bali zinafanya utoaji wa huduma za Posta kuwa za kisasa zaidi Kwa Kasi zaidi na Kwa gharama nafuu
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa huduma za Mawasiliano Wizara Habari Mulembwa Mnaku Amesema kwamba Kuna jumla ya kamati nne zinakutano ikiwemo kamati ya kuangalia uzalishaji na Teknolojia, kamati ya pili ya mkakati wa kuangalia mashirika yanafanyakazi zake Kwa ufanisi huku kamati ya tatu imiangalia Masuala ya sera huku ya mwisho ikiwangalia Masuala ya fedha na rasilimali watu.