Na Ahmed Mahmoud
Mchakato wa mageuzi Makubwa ya Mfumo wa uendeshaji wa Ofisi ya Msajili wa hazina kuendana na soko la uwekezaji limepelekea kuanza mchakato wa kubadili sheria ya uendeshaji wake hadi kukamilika Kwa sheria hiyo mwezi novemba mwaka huu.
Aidha mabadiliko hayo ya muundo wa sheria itapelekea Jina kuwa Mamlaka ya Uwekezaji wa Umma Public Investment Authority (PIA kuendana na hali ya uwekezaji Kwa kushirikisha Umma katika uendeshaji wa mashirika ya Umma.
Akitoa mada ikiwa ni siku ya Pili ya Kikao Kazi cha wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma nchini kinachoendelea Kwa siku Tatu Jijini Arusha Msajili wa hazina Nehemiah Mchechu Amesema kuwa kubadili Muundo na Jina kunaakisi mageuzi kuendana na suala Zima la uwekezaji kurudisha mashirika kujiendesha yenye na kuweza Kutoa Faida Kwa Serikali.
Alisema kwamba upungufu uliomo katika sheria ya Ofisi ya Msajili wa hazina Pamoja na thamani ya uwekezaji kuonekana kubwa Bado uwekezaji huo haukidhi malengo ya msingi ya maeneo muhimu ya Uchumi ikiwemo uwekezaji ndio maana ipo haja ya kubadili muundo.
Kwa mujibu wa Mchechu alieleza kwamba kukosa chanzo Cha uhakika na endelevu Cha mitaji ya uwekezaji ikiwemo wigo finyu wa uwekezaji unaathiri uendeshaji wa shughuli za Serikali Kutoa mitaji Kwa mashirika ya umma.
“Kuna makundi manne yanayotuongoza kwenda kwenye zile R4 za Mh.Rais ambazo sisi tumechukuwa mbili pekee ambazo ni Reform and rebuild kwenda kwenye muundo wenye maana kujenga suala Zima la uwekezaji wenye tija ili kuendesha mageuzi ya mashirika yetu kupata mitaji na kujiendesha Kwa Faida”
Vile vile alisema kwamba kuendana na muundo huo mpya wa mamlaka itasaidia kuboresha usimamizi na ufuatiliaji ikiwemo kuwa na sheria mpya na kujenga upya muonekano wa mabadiliko
Hata hivyo Amesema matumizi ya mashirika kupata mitaji Ili kuwa ni sehemu ya kuishirikisha Umma badala ya Serikali ilivyokuwa inatoa mitaji na kuicha jamii kuwekeza ndio maana Leo yamekuwa ya Serikali badala ya neno umma kutumika kuilenga jamii.
[8/20, 13:21] Ahmed Mahmoud: “Mchakato mzima wa kufikia mabadiliko ya sheria ya Msajili wa hazina yatakamilika mwezi novemba na hivyo tutatoka kuitwa Ofisi ya Msajili wa hazina kwenda kuwa Mamlaka ya Ukewekezaji wa Umma ….. yaani Public Investment Authority (PIA) “