Mabasi ya Kampuni ya Jostano and General Supplises Limited yakiwa Stendi ya Mabasi ya Mkoa wa Singida Misuna tayari kwa safari zake.
……………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Jostano and General Supplises Limited licha ya kuanza kufanya
kazi hivi karibuni imekuwa kinara katika
sekta ya usafirishaji hapa nchini hususani katika Mikoa ya Singida, Manyara,
Morogoro, Dar es Salaam, Dodoma na Mbeya.
Licha ya kuwa na miaka miwili katika sekta hiyo tangu ianze kufanya kazi
zake mwaka 2021 kampuni hiyo imejizolea umaarufu mkubwa kutokana na utoaji wa
huduma zake kwa viwango vya hali ya juu
na kuwa kimbilio la abiria wengi.
Mfanyabiashara Margaret Ntandu ambaye anasafirisha mchele kati ya Mkoa wa
Tabora kupitia Singida anasema amekuwa akisafirisha bidhaa hiyo kupitia mabasi
ya kampuni hiyo na haja wahi kupata changamoto yoyote.
” Nimekuwa nikisafirisha mizigo yangu kutoka Singida kwenda Dodoma
sijawahi kupata changamoto ya aina yoyote iwe ya kupotea mzigo na nyingine na
hata bei zao ni rafiki ukilinganisha na mabasi ya kampuni zingine,” alisema
Ntandu.
Edina Alex ambaye ni mfanyabiashara wa vitenge anayevitoa Tunduma na
kuvipeleka Singida anasema mabasi ya kampuni hiyo ndiyo anayopanda wakati
akifuata bidhaa zake hizo na kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wamekuwa na lugha
nzuri kwa abiria.
Alex anasema tangu kampuni hiyo ianze kufanya safari zake Mkoa wa Mbeya
anatumia mabasi ya kampuni hiyo na akaupongeza uongozi kwa kusimamia vizuri
utendaji kazi wa wafanyakazi ambao umewapa mafanikio hayo kwa kipindi kifupi
tangu waingie kwenye sekta hiyo.
” Niwaombe viongozi wa kampuni hii waendelee kuwa wabunifu kwa kujifunza
zaidi kutoka kwa makampuni yenye uzoefu naamini ndani ya miaka miwili ijayo
Jostano Trans watakuwa wabobezi wakubwa kwenye sekta hii kwani wameanza
vizuri,” alisema Alex.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ] UDSM }, Amina Seif ambaye
alisafiri na basi la kampuni hiyo kutoka Singida kwenda Dar es Salaam alisema
muda wanaoambiwa kufika Dar es Salaam kutoka Singida unakuwa ni uleule wa saa
11 na nusu jioni tofauti na mabasi mengine ambayo yanafika kuanzia saa 12 jioni
hadi saa mbili na kuendelea.
”Abiria waliowengi hawapendi longolongo wanapenda kufika muda uleule
walioambiwa labda tu ziwepochangamoto za kuharibika kwa gari lakini za
kukamatwa na trafiki zinaweza kuepukika kwa kuzingatia sheria za usalama
barabarani kama za mwendo kasi, uchakavu wa gari na matairi,” alisema Seif.
Alisema lugha nzuri wakati wa utoaji huduma kwa abiria ni jambo lingine
ambalo limemfanya avutike na kusafiri kwa kutumia mabasi hayo na utaratibu wa
kuomba dua wakati wa kuanza safari na baada ya kufika.
Wakala wa mabasi katika Stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Awadhi Sendoro alisema amefanya kazi hiyo kwa muda mrefu katika stendi hiyo na kueleza kuwa kampuni hiyo kwa muda mfupi tangu ianze kufanya kazi imekuwa na wateja wengi.
” Mimi sio wakala wa mabasi hayo lakini kutokana na watu wengi kuwa na namba zangu wamekuwa wakinipigia simu niwashikie nafasi katika mabasi hayo na nimekuwa nikifanya hivyo,” alisema Sendoro.
Alisema abiria wengi wamekuwa wakipenda kusafiri na magari hayo kwa sababu ya huduma nzuri wanazozipata na kufika muda wanaoambiwa na mwendo mzuri wa mabasi hayo.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Kampuni hiyo hiyo, Elias Meko alisema mafanikio hayo
waliyoyapata kwa muda mfupi yanatokana na ushirikiano baaina ya viongozi wa
kampuni hiyo pamoja na wafanyakazi ambao wakati wote ndio wanaokuwa na abiria.
” Tumekuwa tukikutana na wafanyakazi wetu wa kada zote wakiwemo makondakta
na madereva na kufanyanao vikao kazi kwa ajili ya kukumbushana majukumu ambayo
matunda yake ndiyo mafanikio haya yanayoonekana kwa abiria tunao wahudumia,”
alisema Meko.
Alisema kampuni hiyo ilianza rasmi kufanya kazi zake mwaka 2021 kati ya
Singida na Babati Manyara na baadae Singida, Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam.
Meko alisema hivi sasa wameanzisha safari ya kutoka Singida kwenda Mbeya na kuwa
kampuni yao hivi sasa imekuwa bora na kimbilio kwa wananchi wanaosafiri kwa
mabasi yao.
Alisema licha ya kuwepo na ushindani wa kibiashara hali sio mbaya hasa
ukizingatia kuwa hawana muda mrefu tangu waingie kwenye sekta hiyo na amewaomba
wananchi kuendelea kuwaamini na kuwaunga mkono zaidi na wao wataendelea kuwapa
ushirikiano lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali chini ya Rais
Dk.Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha sekta ya usafirishaji inakua na kutoa
huduma bora kwa wananchi.
Katibu Mkuu huyo Kiongozi alisema wamekuwa na safari zao kila siku kutoka Singida kwenda Dares
Salaam, Dar es Salaam kwenda Singida, Singida kwenda Mbeya na Mbeya kwenda
Singida na kuwa tiketi zao zinapatikana kwa njia ya mtandao www.jostano.co.tz na www.busbora.co.tz.
Alisema namna ya kununua tiketi zao kwa njia ya mtandao hatua ya kwanza ni
tembelea www.jostano.co.tz au pakua BUSBORA
APP kutoka google play Store busbora.co.tz.
Alitaja hatua ya pili ni kuchagua
unapotoka na unapotaka kwenda na tarehe ya safari kisha ‘TAFUTA’
Meko alitaja hatua ya tatu kuwa Chagua Bus la Jostano Trans kisha ” ONYESHA
SITI” chagua siti uipendayo, chagua
kituo cha kushukia na kupandia. Jaza majina kamili, namba ya simu, jinsi kisha
endelea.
Alitaja hatua ya nne ni hakikisha taarifa za safari yako na kisha ENDELEA
NA MALIPO.
Alitaja hatua ya tano kuwa ni chagua mtandao wa malipo kisha fuata
maelekezo yanayojitokjeza kulipia.
Alitaja hatua ya mwisho kuwa mara baada ya malipo utapokea ujumbe wenye
uthibitisho wa tiketi na utaweza kupakua nakala ya tiketi katika kifaa chako.
Meko alisema vitu vya kuzingatia kuwa ni vigezo na masharti vilivyowekwa ni
nauli iliyowekwa kwenye tiketi haibadilishwi, kuzingatia muda wa safari na
abiria afike kwenye kituo cha kupandia bus kabla ya nusu, mzigo wa ziada
utakaozidi kilo 20 utatozwa nauli, mzigo wa mkononi wa abiria sio dhamana yao, abiria akisitisha
safari atoe taarifa saa 12 kabla ya safari na atakatwa asilimia 15 ya nauli
aliyolipa.
Alitaja vigezo na masharti mengine kuwa ni iwapo abiria atasitisha
safari pasipo kutoa taarifa au kuachwa na basi kwa kuchelewa kufika kituo cha kupanda nauli haitarudishwa.
Alisema viongozi wa kampuni hiyo wapo tayari wakati wote kupokea maoni mbalimbali wanayoletewa na wasafiri wao na kuyafanyia kazi mara moja ikiwa ni ni moja ya njia ya kuboresha huduma zao.
Alisema kila penye mafanikio hapakosi kuwa na changamoto za hapa na pale hivyo aliwaomba wateja wao kuendelea kuwaamini na kwa changamoto zilizojitokeza wakati wa safari zao wanaomba wawasamehe,
Pia Meko ameendelea kuwahimiza wateja wao kukata tiketi kwenye ofisi zao au kwa njia ya mtandao jambo litakalosaidia kuondoa changamoto za kuzidishiwa nauli na kutapeliwa,
Katika hatua nyingine Meko amesema kampuni hiyo itakuwa na uchoyo wa fadhira iwapo itashindwa kumshuru na kuthamini mchango wa Kampuni ya mabasi ya Happy Nation katika mchango mkubwa wa ukuaji wa kampuni yao ya Jostano Trans na kuwa wanashirikiana viziri na Mkurugenzi wa kampuni hiyo ndugu Issa ambaye amekuwa hachoki kushiriukiana nao katika kila jambo la kuboresha utendaji kazi ambao umewaletea mafanikio hayo.
Aidha, alitaja namba za mawakala wao kuwa ni 0683-712030 Makao Makuu
Dar es Salaam, 0765-290928 Singida, 0786-292792 na 0759-500010 Dar es Salaam, 0785-776402
Dodoma , 0655-900909 Morogoro na Mbeya ni 0752-397910.