Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwasilisha wa taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa katika kuhuisha Sheria ya Mazingira (2004) na ya Hali ya Mazingira (2021-2023) kwa Kamati ya Kuhudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, kikao kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 21 Agosti, 2021. Kulia ni Naibu Waziri wake Mhe. Khamis Hamza Khamis na Kaimu Katibu Mkuu Dkt. Switbert Mkama.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Anna Lupembe akifungua kikao cha kupokea na kujadili taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa katika kuhuisha Sheria ya Mazingira (2004) na ya Hali ya Mazingira (2021-2023) kwa Kamati ya Kuhudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, jijini Dodoma
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika kikao cha kupokea na kujadili taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa katika kuhuisha Sheria ya Mazingira (2004) na ya Hali ya Mazingira (2021-2023) kwa Kamati ya Kuhudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, jijini Dodoma
……..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali imeandaa programu na kutekeleza miradi mbalimbali ya usimamizi endelevu wa hifadhi ya ardhi.
Amesema hayo wakati akiwasilisha wa taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa katika kuhuisha Sheria ya Mazingira (2004) na ya Hali ya Mazingira (2021-2023) kwa Kamati ya Kuhudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, kikao kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 21 Agosti, 2021.
Hatua hiyo imekuja kutokana na tatizo la uharibifu wa ardhi ulioathiri baadhi ya maeneo nchini, hivyo Serikali kwa kushirikiana na wadau inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo usimamizi endelevu wa hifadhi ya ardhi katika mikoa ya Kilimanjaro Shinyanga, Tabora na bonde za Ziwa Nyasa.
Dkt. Jafo amebainisha kuwa mradi mkubwa wa usimamizi endelevu wa mifumo-ikolojia ya miombo magharibi mwa Tanzania, miradi ya usimamizi wa ardhi ya Kilombero na Rukwa na usimamizi endelevu wa mfumo ikolojia ya Mlima Kilimanjaro.
Amesema Serikali imewezesha uandaaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa vijiji 2,556 kati ya vijiji 12,318 ambao unasaidia wananchi kupanga namna sahihi ya matumizi ya ardhi bila kuathiri mazingira.
Hata hivyo, amesema uharibifu wa ardhi kwa kiasi kikubwa husababishwa na shughuli za kibinadamu zisizo endelevu zinazosababisha kuondolewa kwa uoto wa asili, upotevu wa udongo na ubora wa udongo.
Ametaja shughuli hizo kuwa ni kilimo kisicho endelevu, ufugaji wa mifugo usiowiana na maeneo ya malisho, shughuli zisizo endelevu za uchimbaji madini, uchomaji moto ovyo.
Dkt. Jafo ametaja changamoto nyingine kuwa ni kuenea kwa viumbe vamizi na ukataji miti ovyo kwa ajili ya mbao, kuni na ujenzi ambavyo huchangia kwa kiasi kikubwa kuondoshwa kwa uoto wa asili.
Maeneo yenye uharibifu mkubwa wa ardhi yamebainika kuwa ni mikoa ya Tabora, Dodoma, Singida, Shinyanga, Lindi, Pwani Simiyu, Manyara, Arusha, na Ruvuma.