Timu ya kata ya Kitangiri imeanza vizuri mashindano ya The Angeline Jimbo Cup 2023 kwa ushindi wa magoli matatu kwa sifuri dhidi ya Timu ya kata ya Nyamanoro mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari Baptist iliyopo Kona ya Bwiru wilayani Ilemela
Akizungumza mara baada ya kufungua mchezo huo, Mgeni rasmi ambae pia ni Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Kitangiri Ndugu Nasoro Mgema amevitaka vilabu shiriki vya mashindano hayo kuhakikisha vinatumia fursa ya uwepo wa ligi ya The Angeline Jimbo Cup 2023 kuonyesha vipaji vyao ili waweze kupata nafasi katika timu kubwa nchini pamoja na kutumia michezo kama sehemu ya ajira na kujenga afya
‘.. Tunamshukuru Mbunge Dkt Angeline Mabula kwa kuanzisha mashindano haya, Kama Vijana tutaamua kuyatumia vizuri yatatusogeza mbele na tutaweza kujikwamua kiuchumi kwani timu nyingi nchini zinatumia wachezaji waliotokana na mashindano haya na wamefanikiwa kiuchumi ..’ Alisema
Aidha Ndugu Mgema amewataka wananchi wa jimbo la Ilemela kumuunga mkono na kumuombea kwa Mungu Mbunge Dkt Angeline Mabula kwa juhudi zake za kuanzisha na kuendeleza mashindano hayo huku akiwataka viongozi wengine kuiga mfano huo
Kwa upande wake Katibu wa Mbunge kanda ya Kirumba Bi Fatma Karoli amezitaka timu shiriki za mashindano ya The Angeline Jimbo Cup 2023 kucheza kwa amani na usalama huku akivipongeza vilabu vya Nyamanoro na Kitangiri kwa kumaliza salama mchezo wao
Eric Mabogo ni nahodha wa timu ya kata ya Kitangiri ambapo amesema kuwa mafanikio ya timu yake yametokana na kujitoa na kujituma kwa wachezaji japo timu pinzani haikuwa mbaya tofauti na udhaifu wa kiufundi waliouonyesha sambamba na kuwaomba mashabiki kuzidi kujitokeza na kuwatia moyo ili waweze kufanya vizuri zaidi
Mpaka tamati ya mashindano hayo Kwa siku ya Leo Timu ya Kitangiri ilifanikiwa kupata magoli matatu la kwanza likifungwa dakika ya 43 na mchezaji Jezi nambari 11 Leonard Maarufu, goli la pili likifungwa dakika ya 51 na mchezaji Jezi nambari 10 Khalfan Mkama na la tatu likifungwa dakika ya 89 na nahodha wa timu hiyo Eric Mabogo Jezi nambari 7 mgongoni
Kesho Jumapili mashindano hayo yataendelea katika uwanja huo Kwa kuwakutanisha watoto wa mjini Timu ya kata ya Kirumba dhidi ya Timu ya kata ya Ibungilo kuanzia saa9.30 alasiri