Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi mbalimbali wakati wa wimbo wa Taifa na Afrika Mashariki alipowasili kwenye Ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha
Viongozi na Watendaji wa Taasisi mbalimbali wakisikiliza na kufuatilia kwa makini Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Tuzo kwa baadhi ya Viongozi wa Taasisi na Kampuni zilizofanya vizuri kwenye kuchangia Maendeleo ya Serikali kwa Mwaka 2021/22, mara baada ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Kasssim Majaliwa kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuleta maendelea nchini , mara baada ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma pamoja na Viongozi mbalimbali mara baada ya kufungua Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023
Julieth Laizer,Arusha .
RAIS wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ,Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kubadilika kiutendaji na kuanza kujitegemea badala ya kuwa mzigo na kuendelea kutegemea serikali.
Ameyasema hayo leo jijini Arusha Arusha akifungua kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kikao cha siku tatu kinachofanyika katika ukumbi wa mikutano wa AICC uliopo mkoani Arusha .
Mhe Samia amesema kuwa,kuna baadhi ya Taasisi nyingi hadi hivi sasa zimekuwa mzigo kwa serikali na kuendelea kutegemea serikali jambo ambalo amewataka kubadilika hivi sasa na kuanza kujitegemea na kuzalisha faida kwa serikali kama ambavyo zinafanya Taasisi zingine.
“Kama mashirika yanatakiwa kujitegemea yenyewe badala ya kutegemea fedha za serikali na nataka kuona fedha hizo zinafanya kazi ipasavyo na kutimiza malengo yaliyokusudiwa. “amesema .
Ameongeza kuwa ,mashirika yanatakiwa yachangie kwa kutoa faida serikalini huku akiyataka mashirika hayo kubadilika na kujiendesha yenyewe ,huku wakijizatiti katika kuzalisha na kutoa huduma kwa faida yao na serikali kwa ujumla.
Aidha ameyataka mashirika hayo kutoka na kwenda nje ya nchi kutafuta masoko na kuweza kuipatia serikali faida serikali ,na kuwataka kujipanua zaidi hadi nchi za nje kama ambavyo CRDB wamefanya.
Mheshimiwa Samia amewataka Wenyeviti wa bodi na watendaji kuhakikisha wanasimamia mashirika hayo kikamilifu na kutumia fedha za serikali kwa umakini kwani serikali inatumia fedha nyingi sana na sasa hivi serikali haina utani kwenye swala la fedha tena.
Naye Waziri ofisi ya Rais .mipango na uwekezaji,Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa,kumekuwepo na usimamizi mabovu kwa Wenyeviti wa bodi katika kusimamia taasisi zao ha hivyo kusababisha kuleta hasara na kushindwa kuipatia faida serikali.
“Ni wakati wa kubadilika kwa Taasisi hizi kwani utendaji huu unashusha ufanisi wa utoaji huduma kwa jamii na kuendelea kuiletea serikali hasara ,taasisi zilizo goigoi lazima ziondolewe kwani zimekuwa kikao kikubwa kwa maendeleo ya nchi.”amesema Kitila.
Kwa upande wa Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu ametaka uwepo wa maboresho ya Utendaji katika Uendeshaji wa Mashirika ya Umma nchini ili kwendana na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Amesema kuwa,lengo la kukutana Wakuu wa Taasisi za Umma na Wenyeviti wa bodi ni kujadiliana Utendaji wa Mashirika hayo ili kuongeza ufanisi mkutano ambao unashirikisha pia baadhi ya mawaziri na Makatibu wakuu.
Mchechu amesema mkutano huo wa siku tatu unalengo la kuwakutanisha Watendaji wa Taasisi za Umma Serikali ni kuboresha Utendaji kazi na kuongeza zaidi ufanisi.
Mchechu amesema,Ofisi ya Hazina imeandaa mkutano huo ambao utakuwa ukifanyika kila mwaka ili kuboresha Utendaji wa Taasisi za Umma lakini pia kuja na mabadilikoambayo yataongeza ufanisi na kufikia malengo ya serikali.
“Kikao hiki ni nafasi za kuzungumza changamoto zetu na kujadiliana jinsi ya kuzitatua kwa pamoja kwani taasisi zetu zinamahusiano ya karibu”amesema Mchechu.
Mkutano huo wa siku tatu unaendeleaje katika kituo cha mikutano Cha Arusha AICC ukiwakitanisha Mawaziri,Makatibu wakuu,watendaji wa Serikali na wajumbe wa bodi za Mashirika ya Umma na Taasisi zake .