Na Lucas Raphael,Tabora
Mkazi wa kijiji cha Mhungulu Mwangohe Wilayani Nzega Mkoani Tabora Amosi Matias (35) amenusurika kifungo cha maisha jela baada ya kukiri kosa na kutoisumbua mahakama na hivyo kutumikia kifungo cha miaka 15 .
Hukumu hiyo itolewa jana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora ,Athumani Matuma baada ya kukiri kumfanyia upasuaji wa sehemu za siri na tumbo Lukwaja Selemani (78) mkazi wa kijiji cha Mhungulu Mwangohe Wilayani Nzega Mkoani Tabora na kusabisha kifo .
Alisema kwamba ameamua kutoa hukumu hiyo ndogo kwa mshitakiwa baada ya kutia hatianai kufuatia kusababisha mauaji pasipo kuwa na vibali vyoyoyte vinavyomuonesha kuwa yeye ni Daktari wa binadamu.
Hata hivyo Jaji huyo alisema kwamba mshitakiwa hakuweza kuisumbua mahakama hiyo kwa kukiri kufanya utapeli huo hivyo dhabu yake ilikuwa kutoa kifungo cha maisha jela hadi kutumikia miaka 15 jela.
Jaji huyo aliendelea kusoma hukumu hiyo alisema kwamba Mshitakiwa awali alikiri kutenda kosa hilo la kufanya upasuaji kwa mzee huyo sehemu mbili za mwili wake akiwa amemlaza kwenye kitanda cha Udongo wa Tope.
Alisema amesikiliza hoja 8 kutoka kwa Wakili upande wa utetezi Ikram Msomi ambapo sita zillilkataliwa na zingine hoja 4 kukataliwa kwa wakili wa Serikali Mmari Mmari ambazo ikiwa mahakama itende haki kutokana na kosa alilolitenda Mshitakiwa.
Aidha Jaji huyo alisema Mahakama imetoa adhabu hiyo ni haki kwa kupitia kifungu cha mauaji cha 196 na cha 197 na kuonyesha mwenendo mzima wa mshitakiwa kufanya Upasuaji kwenye sehemu za siri na tumbo la marehemu bila ya kuwa na cheti kinachoonyesha kama yeye ni daktari.
Hata hivyo alisema kwamba ili kuipatia hadhi mahakama katika jamii kuweza kuheshimika katika makosa ya mauaji ni hatua ya adhabu zitolewe kutokana na kosa la mshitakiwa.
“Yaani Mkoa wa Tabora Unapaswa kusaidiwa kisheria ili wananchi wajiepushe na Madaktari Feki ambao wanaweza kuwapotezea maisha yao na familia zao “alisema jaji
Awali wakili wa upande wa Jumhuri ukiongozwa na Mmari Mmari aliambia mahakama kuu kwamba Mshitakiwa alitenda kosa hilo mnamo juni 10 mwaka 2022 katika kijiji hicho akijifanya yeye ni daktari bila ya kuwa na kibali chochote kinachomtambulisha kuwa yeye ni Daktari .
Alibainisha kwamba Mshitakiwa huyo alikuwa akitoa tiba ya kuwang’oa meno wananchi kwa malipo ya shilingi elfu 15 ,upasuaji ni 200,000 ambapo awali alitanguliziwa 150,000 ,baada ya kufariki marehemu wanafamilia hawakuweza kumlipa fedha zozote na kuwazalisha akina mama huku katika chumba cha kuwalaza wagonjwa kuna kitanda cha udongo wa tope.
Alisema mshitakiwa huyo alikuwa anawapotosha wananchi na kuwapeleka njia isiyo kuwa sahihi kwa kuwa hakuwa na leseni wala kibali kinachoonyesha kuwa yeye ni daktari wa binaadamu.