Na MJJWM, Mbeya.
Jamii imeaswa kuacha hulka na tabia yakuwalea watoto kwa hofu, vitisho na vipigo, kwani hali hiyo inampunguzia mtoto kujiamini awapo mtu mzima.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, amesema hayo Julai 06, 2023 lwenye Maonesho ya Nane Nane yanayo endelea mkoa Mbeya katika Viwanja vya John Mwakangale.
Kingale pia ameitaka jamii kuwajenga Watoto kwenye malezi yasiyo na hofu wakati wa wa hatua za Makuzi ili kuwa raia wema na wenye kujiamini ndani ya jamii
Akiwa kwenye Banda la Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum amenukuliwa akisema
“Ni ukweli kwamba, jamii ikiwajenga watoto katika kujiamini na kujisimamia wakati wa utoto wao wtawawezesha kujiamini hata wanapokuwa watu wazima na kufanya maamhzi sahihi” amesema Kigahe.
Aidha Kigahe ametumia nafasi hiyo kuipongeza WiZara kwa juhudi inazochukuwa hususan katika kukabiliana na Vitendo vya ukatili na kusisitiza kwamba, jamii ikiwa na ukatili hata shughuli za uzalishaji Mali haziwezi kuendelea wala kufanikiwa.
Awali Afisa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Regina Molel, alimuelezea Naibu Waziri huduma zinazo tolewa na Wizara hiyo ikiwepo huduma za Msaada wa Kisaikolojia, Uwezeshaji wanawake kiuchumi na usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
“Sisi kama Wizara tunashiriki Maonesho haya kwa Mara pili Mfululizo hivyo, tunajitahidi sana watu waelewe shughuli zetu ikiwepo Usimamizi wa Taasisi zetu mbili na vyuo Nane vya Maendeleo ya Jamii ” amesema Regina.
Mbali na Naibu Waziri kutembelea Banda hilo la Wizara watu na Makundi yalio tembelea ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mhe. Beno Malisa ambaye ameiomba Wizara kuendelea kutoa elimu yakupinga ukatili kwa watembeleaji wa Maonesho hayo.
Ikiwa ni Siku ya Sita tokea kuanza kwa Maonesho hayo, Viongozi wa Shujaa wa Maendeleo ya Ustawi wa Jamii mkoa wa Mbeya nao walifika katika banda hilo la Wizara na kutoa elimu kwa jamii iliyokuwepo katika Banda hilo.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ni moja ya Wizara ianayoshiriki Maonesho hayo ambayo yanafanyika mkoani Mbeya kwa Mara ya pili mfululizo.