Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu ametaka kuwepo kwa juhudi zaidi kwa ajili ya kuongezeka kwa idadi ya viongozi wanawake katika idara mbalimbali kuanzia ngazi za chini hadi juu ili kuendelea kuchochea maendeleo zaidi.
Ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa wabunge wanawake kutoka mabunge ya nchi za Afrika wanachama wa jumuiya ya madola unaofanyika jijini Arusha.
Samia amesema kuwa,kwa sasa hivi kuna mawaziri wanawake wapatao 7 kati ya mawaziri 23 na manaibu Waziri wanawake 4 kati ya manaibu 22,hivyo kufanya wawakilishi wanawake bungeni kufikia asilimia 24.4,hivyo kufanya takwimu hizi kuwa kubwa kuliko nchi zingine.
Naye makamu mmoja wa viongozi wa chama hicho bintu jalia alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuangalia nafasi ya mwanamke katika mchakato wa uchaguzi
Alisema kuwa wanawake wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika nafasi za uchaguzi na hawapaswi kuwa na hofu kwa jambo lolote
Alifafanua kuwa kuna manufaa makubsa sana kwa jamii kupata kiongozi ambaye ni mwanamke kwa kuwa anapokuwa kiongozi anaweza kutoa mchango ambao ni mkubwa sa na hivyo manufaa kurudi kwa jamii yake
Awali mbunge kutoka katika bunge la tanzania bi mboni mhita alisema kuwa wanawake wenye ndoto za uongozi hawapasi kukata tamaa hata kama watakutana na magumu kiasi gani
Mboni alitolea mfano kwake yeye mwenyewe kuwa alisha shiriki katika nafasi za uongozi zaidi ya mara 6 na kuanguka lakini haikuwa sababu ya yeye kukata tamaa alipambania mpaka alipopata hivyo wanawake hawapaswi kukata tamaa kwenye utafutaji wa nafasi za uongozi