Meneja wa kanda ya kati na kaskazini kutoka kampuni ya Agricom Africa Ltd ,Peter Temu akizungumza katika maonyesho ya nanenane yanayofanyika viwanja vya Themi Njiro.
Meneja wa kanda ya kati na kaskazini kutoka kampuni ya Agricom Africa Ltd ,Peter Temu , akionyesha teknolojia hiyo mpya ya Trekta aina ya Kubota katika viwanja vya nanenane Themi Njiro
Julieth Laizer,Arusha .
Arusha .Kampuni ya Agricom Africa Ltd ambao ni wasambazaji wa zana za kilimo Tanzania wamekuja na teknolojia mpya ya trekta aina ya Kubota ambayo inamwezesha mkulima kuweza kurahisisha shughuli zake za kilimo kwa haraka na kwa kutumia matumizi madogo ya mafuta.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Meneja wa kanda ya kati na kaskazini,Peter Temu wakati akizungumza katika maonyesho ya nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Themi Njiro.
Amesema kuwa,wamekuwa wakimsaidia mkulima kuanzia kuandaa shamba hadi kufikia hatua ya kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia mbalimbali za kisasa na kuwawezesha wakulima kuondokana na matumizi ya zana za kilimo za zamani na kuweza kutumia sana za kisasa ambazo zimekuwa zikiongeza uzalishaji kwa kiwango kikubwa .
Temu ameongeza kuwa ,teknolojia hiyo mpya ni sawa na kutumia trekta mbili kwa wakati mmoja kutokana na utalaamu mkubwa ulivyotengenezwa na ni maalumu kwa ajili ya matumizi ya kilimo hasa kwa ukanda wa kaskazini kwani ndo teknolojia sahihi ya kutumia katika ukanda huu.
Amefafanua kuwa ,wana viambata vya kuvunia na kulimia pia ambapo wanataka
kuwasaidia wakulima wa kanda ya kaskazini kuweza kufanya vizuri zaidi na watarajie kupata faida kubwa kwani teknolojia hiyo ni ya nchini Japan na ina ubora wa hali ya juu huku lengo kubwa wakitaka mkulima apate faida zaidi kutokana na kile anachokifanya .
“Tunawaomba wakulima wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kutumia teknolojia hii mpya ya kilimo kwani inatumia mafuta kidogo sana tofauti na trekta zingine na hivyo kumrahisishia mkulima kuweza kumudu gharama wakati wa kilimo na kuweza kufanya vizuri zaidi kwenye kilimo kwa ujumla.”amesema .
Aidha ameongeza kuwa,teknolojia hiyo ina ubora mzuri kwa matumizi ya kilimo kwa wakulima hivyo ni vizuri wakulima watarajie kupata faida zaidi na kumwinua kutoka zana za zamani na kurudi kwenye zana ya kisasa.
Amewataka wakulima kufika kwa wingi katika banda hilo kujionea na kupata elimu juu ya teknolojia hiyo mpya ambayo itawawezesha kuondokana na kilimo cha mazoea na hatimaye kulima kilimo chenye tija.