Mkuu wa kiwanda cha Samani -Magereza Arusha ,Mrakibu wa Magereza, SP Baraka Muhoho akizungumza katika maonyesho hayo jijini Arusha
Mkaguzi wa magereza kitengo cha Kilimo -Moshi ,Malinda Chilo akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea katika banda hilo la Magereza katika viwanja vya nanenane vilivyopo Themi -Njiro .
Julieth Laizer,Arusha .
Wananchi kutoka kanda ya kaskazini wameshauriwa kutembelea katika maonyesho ya nanenane kwa ajili ya kujifunza maswala mbalimbali ya kilimo,uvuvi na ufugaji na kuweza kujionea teknolojia zilizopo kwa lengo la kuboresha shughuli zao pamoja na kuweza kujiajiri .
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mkuu wa kiwanda cha Samani -Magereza Arusha ,Mrakibu wa magereza SP Baraka Muhogo wakati akizungumza katika maonyesho ya 39 ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro.
Amesema kupitia maonyesho hayo wamekuwa wakionyesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kiwanda hicho zikiwemo samani za maofisini na hata majumbani.
Ameongeza ,wamekuwa wakitoa mafunzo ya ufundi namna ya kutengeneza samani hizo kwa wafungwa waliopo gerezani ambao mwisho wa siku huwawezesha kupata ujuzi ambao huenda kuutumia pindi wanapomaliza kifungo na kwenda kuwa mafundi mahiri wa kutengeneza zamani zenye ubora wa hali ya juu.
“tunatengeneza bidhaa imara sana na bei zetu ni nafuu sana ambazo zinamwezesha kila mmoja kuweza kumudu gharama kwani bidhaa zetu zinadumu kwa muda mrefu ,hivyo tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kuangalia bidhaa zetu pamoja na kuzinunua pia kwani zina ubora wa hali ya juu “.amesema
Naye Mkaguzi wa Magereza kitengo cha kilimo Moshi,Malinde Chilo amesema wamekuwa wakijishughulisha na kilimo cha mboga za matunda, mboga za majani na mahindi kwani wanajali vijana zaidi kwani ni nguvu kazi inayotumika katika kuzalisha mazao kwa tija na kuweza kukidhi katika eneo la chakula .
Amefafanua kuwa, wanafundisha namna ya kuweza kulima nyanya katika eneo dogo na kuzalisha kwa wingi ambapo wamekuwa wakifundisha wafungwa namna ya kulima kilimo bora na kupata faida nzuri kupitia kilimo hicho.
Amesema kuwa, wamekuwa wakulima mazao tofauti na kuwakutanisha wakulima na kuweza kujifunza naomna ambavyo Magereza wamekuwa wakilima kisasa na wamekuwa wakitoa elimu hiyo kwa wananchi bure.
Aidha amewataka wananchi mbalimbali kujitokeza kwa wingi kufika kwenye maonyesho hayo hususani katika banda la Magereza na kuweza kupata elimu mbalimbali na kuweza kujifunza zaidi kuhusu ufugaji na kilimo bora chenye tija.