Kaimu Kiongozi wa msafara wa timu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa, Ndg. Edmund Mugasha akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa chama cha National League for Democracy (NLD) walipofika katika Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Tandika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa NLD, Ndg. Tozy Ephraim Matwanga na wapili kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Ununuzi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa , Bibi. Edna Assey.
Katibu Mkuu wa chama cha National League for Democracy (NLD), Ndg. Tozy Ephraim Matwanga akifafanua jambo mbele ya wajumbe toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa waliofika katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho kwa lengo la kufanya uhakiki wa chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa ni takwa la kisheria lenye lengo la kufuatilia utekelezwaji wa sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bi. Dina Mcharo akielezea jambo wakati zoezi la uhakiki wa chama cha National League for Democracy (NLD) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa NLD, Ndg. Tozy Ephraim Matwanga, Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa NLD(jina lake limehifadhiwa), Mkuu wa kitengo cha Ununuzi Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa , Bibi. Edna Assey na Kaimu Kiongozi wa msafara wa timu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa, Ndg. Edmund Mugasha.
Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakikagua baadhi ya nyaraka za chama cha National League for Democracy (NLD) wakati wa zoezi la uhakiki wa chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwanasheria, Dina Mcharo, Afisa Utumishi, Eneja Mwakanyamale, Afisa Ugavi, Shangilio Mbosa na Afisa Mipango, Kelvin Swai.
Katibu Mkuu wa chama cha National League for Democracy (NLD), Ndg. Tozy Ephraim Matwanga akitoa maelezo kuhusu kadi ya uanachama mbele ya wajumbe kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa waliofika katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho kwa lengo la kufanya uhakiki wa chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwanasheria, Bi. Dina Mcharo, Edmund Mugasha na Edna Assey. Zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa ni takwa la kisheria lenye lengo la kufuatilia utekelezwaji wa sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Timu ya maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha National League for Democracy (NLD) mara baada ya kumaliza zoezi la uhakiki katika chama hicho leo jijini Dar es Salaam. (Picha na: ORPP)
…………………………………….
Na Sophia Kingimali
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Tanzania imetoa Rai Kwa vyama vya siasa kujiendesha Kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo ndani ya Ofisi hiyo, Kwani lengo la ofisi hiyo kuona vyama hivyo vinajiendesha kama taasisi hivyo kila chama kinatakiwa kifuate taratibu zilizopewa alipokuwa anasajili chama.
Akizungumza na fullshangwe kwenye zoezi hilo Agosti 3 jiji Dar es Salaam na Ofisa Habari wa Ofisi ya Msajili wa Vyama hivyo, Abuu Kimario amesema vyama vya Siasa vikijiendesha kwa kufuata taratibu zilizopo hakutakuwa na migogoro ndani ya vyama vyao.
“Vyama vya Siasa vifuate taratibu na sheria zilizopo ili kuondoa migogoro ndani na nje ya vyama vyao,”amesema Kimario.
Amesema kazi ya uhakiki si kutafuta mchawi ila inataka kujua uhai wa chama na kama kinafuata taratibu zilizopo katika muongozo wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Amesema kabla ya kazi ya uhakiki tayari walishatuma madodoso katika vyama vyote vya siasa nchini hivyo maswali wanayowauliza tayari wanayajua.
“Hakuna swali geni tunalowauliza tayari yote yapo katika dodoso tuliowatumia awali,” ameongeza.
Aidha Kimario amesema hivi karibuni ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG)ilionyesha baadhi ya vyama vimepata hati chafu katika mahesabu.
Amesema hati chafu hiyo ilisababishwa na kukosa elimu ya kutunza mahesabu lakini tayari Ofisi ya Msajili ilishatoa Elimu baadhii ya vyama na baadhii ya vyama vilikuwa havina tin namba lakini hivi sasa wapo katika utaratibu wa kuipata.
Amesema kazi ya uhakiki hufanyika kila mwaka nchini,lengo ni kuangalia utekelezaji unaofanyika katika vyama hivyo.
“Kazi kubwa ya uhakiki ni kuangalia yale masharti,taratibu na sheria zilizopo zinafuatwa ndani ya vyama vya Siasa vilivyosajiliwa?”amesema
Naye, Mwenyekiti wa chama Cha kijamii cha cck Mchungaji David Mwaijojela aliishukuru Ofisi hiyo kuwafanyia uhakiki na kuwaelimisha baadhii ya vitu ambayo walikuwa hawavifahamu ndani ya chama chao.
Mchungaji Mwaijolela amesema,wanaiomba Serikali iwapatie ruzuku waweze kuendesha Chama chao vizuri.
Uhakiki huo ulianza Agosti 2 mwaka huu ambapo agost 3 imehakiki vyama viwili chadema na CCK.