Kamishna wa Elimu Lyabwene Mtahabwa (wa kwanza kushoto) akika utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) leo tarehe 28 Julai,2023 jijini Arusha.
Kamishna wa Elimu Lyabwene Mtahabwa akisisitiza jambo katika hafla uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Afrika Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete akiongea na wajumbe waliohudhuria uzinduzi rasmi wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) wa taasisi hiyo leo tarehe 28 Julai,2023.
Kamishna wa Elimu Lyabwene Mtahabwa (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela mara baada ya uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) leo tarehe 28 Julai ,2023.
Na Mwandishi wetu
Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia imezindua Kamati ya Ushauri wa Viwanda kwa lengo la kuangalia mambo mbalimbali yatakayoinua uchumi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo leo tarehe 28 Julai, 2023 Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa alisema endapo wanasayansi wabobezi wakifanya tafiti vema wataweza kutatua changamoto za ajira ikiwemo kujua viwanda vinataka nini ili kuwezesha vijana kupata fursa za ajira na kujikwamua kiuchumi.
“Ukiwa mwanasayansi usiache mila na desturi za kitanzania,fanyeni bunifu zenu na kuleta maendeleo katika nchi ikiwemo kujua viwanda vinataka nini na ninyi kufungua fursa kwa vijana ” alisema Kamishna Dkt. Lyabwene Mtahabwa
Naye Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Cha Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete alisema kamati hiyo italeta chachu katika utengenezaji wa mitaala na kujibu changamoto za viwanda na jamii, ambayo ni hatua kubwa ya kubadilisha fikra za watafiti.
“Zile bunifu na gunduzi zibadilishwe na kuwa biashara pamoja na bidhaa zinazozalishwa kutokana na utafiti lazima sasa chuo chetu kisonge mbele katika kukuza sekta ya ajira ” alisema Profesa Anthony Mshandete
Wakati huo huo, Profesa Suzana Augustino ambaye ni Mkuu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) aliongeza kuwa, mradi huo unalenga kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa elimu ya juu.
Profesa Suzana anazidi kueleza kuwa mradi huo unalengo la kubadili mitaala ili wataalam watakaozalishwa kutoa mchango kwa taifa na jamii, ikiwemo uboreshaji wa mifumo ya Tehama katika kufundisha na kufanya tafiti na kuleta maendeleo ya teknolojia na ubunifu nchini Tanzania.
“Tunataka mifumo yetu itoe shahada za uzamili na uzamivu kwa kutumia tehama popote mwanafunzi atakapokuwepo ndani na nje ya nchi, ikiwemo mageuzi makubwa katika maabara na kupewa udhibiti ili kupokea kazi zinazotoka nchi mbalimbali na kusaidia kuzichakata katika masuala nishati,udongo,tafiti na tehama”alisema Profesa Suzana
Aliongeza kuwa, kamati hiyo itatoa ushauri zaidi katika kufikia jamii hususani sekta binafsi viwandani ambapo kumekuwa na tofauti kubwa sana kati ya watafiti na kwenye viwandaili kuhakikisha teknolojia zinazozalishwa zinafika kwa jamii na sekta ya viwanda, katika kuchangia maendeleo ambayo taifa inahitaji katika kupata mpango mkakati wa maendeleo ifikapo mwaka 2050.