Na John Walter- Arusha
Kiongozi wa mila ya wamasai nchini Tanzania ,(Laigwanani) Isaac Ole Kisongo ameunga mkono uwekezaji kwenye Bandari ya Dar es Salaam, akiwataka watanzania kupuuza wanaokosoa Mpango huo wa serikali.
Akizungumza jijini Arusha leo Julai 22,2023 katika Mkutano wa Chama cha Mapinduzi Kanda ya kaskazini uliolenga kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama hicho kikuu nchini Tanzania, uliozungumzia pia Uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Kisongo amesema kuwa Uwekezaji huo utakuwa na tija Kubwa kwa nchi hivyo ni suala la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan badala ya kulalamika.
“Mimi nikiwa kama Kiongozi wa Mila wa Wamasai nchi nzima, nimemuelewa Vizuri Rais Samia na tutampa ushirikiano wa kutosha” alisema Ole Kisongo
Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya sita imefanya mambo Makubwa katika sekta ya Elimu,Afya na hata miundombinu ya Barabara hivyo Uwekezaji huo utaongeza fedha nchini na kuwezesha miradi mingine kufanyika zaidi.
Amesema wanaobeza Uwekezaji huo wana nia ovu na kila mmoja anatakiwa kuwapinga vikali.
Kwa upande wake Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema mwekezaji Kampuni ya DP World atapewa Magati machache na sio yote kama inavyoelezwa kwenye mitandao ya kijamii.