RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mhe. Mahmoud Mohammed Mussa, alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja, kuhudhuria hafla ya Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, kuhudhuria Kilele cha Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar, yaliyoadhimishwa leo 22-7-2023 katika ukumbi huo na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sheria,Katiba,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa.
MSAANII Albajoun Rashid akisoma Shairi Maalum la kuadhimisha Kilele cha Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar, wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh. Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar
BAADHI ya Viongozi mbalimbali wa Serikali na Dini wakifuatilia hutuba wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar, yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanziba
MJUMBE wa Bodi ya LSF Mhe.Jaji Mstaafu Robert Makaramba akizungumza na kutowa salamu za taasisi yake wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar, yaliyoadhimishwa katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar
MKURUGENZI wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Mhe. Hanifa Ramadhan Said akizungumza katika hafla ya Kilele cha Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar, yaliyoadhimishwa katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Kilele cha Maadhinisho ya Nne ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar 2023, yaliyoadhimishwa katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 22-7-2023.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika Kilele cha Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar 2023, maadhimisho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar
WANANCHI wakihudhuria Kilele cha Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar 2023, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi TUZO Bora ya Wasaidizi wa Sheria katika Masuala ya Watu Wenye Ulemavu (Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja NAPAC )Bi. Hamida Ali Makame, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar 2023, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh. Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi TUZO Bora ya Gazeti na Blog katika masuala ya Wasaidizi wa Sheria Ndg. Haji Nassor, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Msaada wa Kisheria Zanzibar 2023, yaliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh. Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 22-7-2023, (kulia kwake) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)