**************************************
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christiopher Olesendeka ametoa mwezi mmoja na nusu kwa wadaiwa sugu wa vyama vya ushirika kurejesha fedha walizokopa na kushindwa kurejeshwa katika muda wa mkataba na kutoa onyo kwa atakayeshindwa kufanya hivyo kufikishwa katika katika vyombo vya sheria.
Mkuu wa mkoa ametoa muda huo kwa wadaiwa sugu wa AMCOS na SACOS za wilaya hizo mbili mara baada ya kukutana nao katika ukumbi wa chuo cha maendeleo mjini Njombe kwa lengo kufanya mahojiano na wadaiwa pamoja na kuweka makubaliano ya lini ya kulipa fedha hizo ambazo wamekaa nazo muda mrefu na kusababisha vyama vingi kufa na vingine kuteteleka.
Akizungumza na wadaiwa hao akiwa na kikosi kazi ambacho ameunda kwa ajili ya kufatilia fedha za NJOCOBA na Vyama vya ushirika ambavyo vimeathirika kwasababu ya madeni makubwa Olesendeka amesema zaidi ya bil 4.5 zipo mifukoni mwa wachache pamoja na bil 1.5 za NJOCOBA ambazo zimekopwa na kushindwa kurudishwa hivyo anatoa mwezi mmoja na nusu kwa wadaiwa kurejesha fedha za ushirika pamoja na wiku 2 kwa wadaiwa wa Njocoba kurejesha.
Kufuatia agizo hilo kwa wadaiwa , Kisha Olesendeka anatoa agizo kwa wakurugenzi,wakuu wa wilaya pamoja na viongozi wa vyama vya ushirika kuhakikisha wadaiwa wote watambuliwa ili waweze kufatiliwa endapo wakippuuza agizo la serikali.
Katika kikao hicho wanadaiwa wanapata fursa ya kutoa mapendekezo na ahadi zao kwa serikali juu ya namna ya kurejesha fedha hizo ambapo wanaomba kupewa muda wa miezi mitatu kwa kuwa wana nia ya kulipa fedha hizo
Deni la bil 4.5 katika vyama vya ushirika linafanya kiasi cha zaidi ya bil 6 kuondoka katika mzunguko wa fedha ambapo katika benki ya NJOCOBA inaelezwa bil 1.5 zilikopwa na hazirejeshwa mpaka benki inaingia mufilisi.