Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.John Jingu,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024 uliofanyika leo Julai 18,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bi.Siti Abbas Ali,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024 uliofanyika leo Julai 18,2023 jijini Dodoma.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Nchini Dkt.Nandera Mhando,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024 uliofanyika leo Julai 18,2023 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mpango Sera na Utafiti Bw.Mussa Shauri Kombo,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024 uliofanyika leo Julai 18,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii OR-TAMISEMI Bi.Subisya Kabuje,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024 uliofanyika leo Julai 18,2023 jijini Dodoma.
Meneja wa Methodolojia za Takwimu na uratibu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw.Emilian Karugendo,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024 uliofanyika leo Julai 18,2023 jijini Dodoma.
Mtalaam wa Afya ya Jamii Dkt.Mubaruk Amri,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024 uliofanyika leo Julai 18,2023 jijini Dodoma.
Mtaalam wa ulinzi wa watoto kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), Evance Mori ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024 uliofanyika leo Julai 18,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dk.Redempta Mbatia,akizungumza wakati wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024 uliofanyika leo Julai 18,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.John Jingu (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024 uliofanyika leo Julai 18,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.John Jingu,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024 uliofanyika leo Julai 18,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imewataka wadau mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya utafiti wa ukatili dhidi ya watoto (VACS) 2024 kuzingatia weledi ili kubaini kiini chake na namna ya kudhibiti.
Hayo yamebainishwa leo Julai 19,2023 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. John Jingu wakati akifungua kikao cha wadau cha kujadiliana na kukubaliana mikakati ya kufanya utafiti huo.
Dkt. Jingu amesema kwakuwa utafiti ni nyenzo muhimu ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto ni wajibu kwa kila mdau kufanya kwa kufuata maadili .
”Ipo haja ya kufanya utafiti huo ambao utasaidia kupata taarifa sahihi zitakazowezesha kupambana na ukatili dhidi ya watoto kwakuwa ni rasilimali muhimu katika taifa.”amesema Dkt.Jingu
Ameeleza kuwa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO) zinaeleza kuwa mwaka jana kwa dunia takribani watoto bilioni moja walifanyiwa ukatili.
”Bara la Afrika zilionesha kuwa takribani asilimia 50 ya watoto walifanyiwa ukatili jambo ambalo halikubaliki ni lazima walindwe.”
Dkt.Jingu amesema kufanyika kwa utafiti huo kutawezesha jambo hilo kujulikana kwa ukubwa, madhara na namna ya kulitatua kwakuwa ili kukabiliana na vita yoyote ni lazima uwe na taarifa sahihi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Zanzibar, Siti Abbas Ali amesema kuwa licha ya kazi kubwa ya kudhibiti suala hilo kuwepo, bado ukatili upo hivyo kupitia utafiti huo watajua changamoto ni zipi na namna ya kuzikabili.
”Takwimu ni suala la muungano na kwamba ofisi ipo tayari kutoa utaalam wake wa uchakataji, ukusanyaji, na usambazaji takwimu zitakazotolewa kupitia utafiti huo.”amesema
Naye Mtaalam wa ulinzi wa watoto kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), Evance Mori amesema lengo la utafiti ni kuhakikisha mtoto analindwa hivyo lazima ziwepo taarifa sahihi na kwamba ni njia mojawapo ya kuelewa ukubwa wa tatizo.