Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, mara baada ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Liwiti inayojengwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia mradi wa SEQUIP.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na walimu, wananchi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Boma yanayojengwa kupitia mradi wa BOOST kwenye halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akipanda mti katika shule ya Msingi Kunduchi, mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa kupitia mradi wa BOOST katika shule hiyo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo kwa walimu na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, wakati akikagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu inayojengwa katika Manispaa hiyo kupitia mradi wa SEQUIP.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akivishwa skafu na mwanafunzi wa Shule ya Msingi Boma, mara baada ya kuwasili katika shule hiyo kwa ajili ya kukagua ujenzi wa madarasa yanayojengwa kupitia mradi wa BOOST kwenye shule hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akielekea kukagua miundombinu ya elimu katika shule ya Msingi Kunduchi inayojengwa kupitia mradi wa BOOST katika shule hiyo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akisalimiana na wananchi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari Liwiti inayojengwa katika Halmashauri hiyo ya jiji kupitia mradi wa SEQUIP.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na wananchi na watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mbele ya jengo la Shule ya Sekondari Liwiti inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP mara baada ya kulikagua jengo hilo.
Na: James Mwanamyoto (OR-TAMISEMI)
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuna ulazima wa kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa shule ili kukidhi mahitaji yanayotokana na ongezeko la wanafunzi ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto wa wanafunzi kutembea umbali mrefu.
Mhe. Ndejembi ametoa wito huo akiwa mkoani Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu inayojengwa kupitia mradi wa BOOST na SEQUIP katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Mhe. Ndejembi amesema maeneo hayo yakitengwa, kuna ulazima wa kujenga shule za ghorofa badala ya majengo ya chini ili kutatua changamoto ya kukosa viwanja vya michezo vya watoto ambavyo ni muhimu kwa ajili ya kujenga afya ya akili.
“Michezo ni muhimu kwa ajili ya afya ya akili na makuzi ya watoto hivyo ni lazima kuwepo na ushirikiano wa viongozi kuanzia ngazi ya mtaa, kata, halmashauri, wilaya na mkoa katika kuhakikisha shule zinajengwa kwenda juu ili kupata maeneo ya viwanja vya michezo,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Ameongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuboresha elimu ya msingi na sekondari, hivyo ni lazima kuendelea kutenga maeneo ya ujenzi na kuyatumia vizuri ili yawe na tija.
Aidha, Mhe. Ndejembi ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kukamilisha ujenzi wa shule mpya na ukarabati wa miundombinu ya elimu, kupitia fedha za mradi wa BOOST na SEQUIP zilizopatikana kutokana na jitihada za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kuendelea kuboresha miundombimu ya elimu nchini.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa miundombinu ya elimu kupitia mradi ya BOOST na SEQUIP na kuahidi kuendelea kusimamia vizuri matumizi ya fedha hizo ili ziwe manufaa kwa taifa.