Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Uongozi kwa Makatibu Tawala wa Wilaya Tanzania Bara yaliyoanza leo Julai 4 hadi Julai 6,2023 katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi jijijni Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati akifungua Mafunzo ya Uongozi kwa Makatibu Tawala wa Wilaya Tanzania Bara yaliyoanza leo Julai 4 hadi Julai 6,2023 katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi jijijni Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Makatibu Tawala wa Wilaya Tanzania Bara yaliyoanza leo Julai 4 hadi Julai 6,2023 katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi jijijni Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angellah Kairuki,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Makatibu Tawala wa Wilaya Tanzania Bara yaliyoanza leo Julai 4 hadi Julai 6,2023 katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi jijijni Dodoma.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mafunzo ya Uongozi kwa Makatibu Tawala wa Wilaya Tanzania Bara yaliyoanza leo Julai 4 hadi Julai 6,2023 katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi jijijni Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa,amewataka Makatibu Tawala wa Wilaya(DAS) kuzingatia miiko na maadili ya viongozi wa umma ili kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Julai 4,2023 jijini Dodoma wakati akifungua semina elekezi kwa Makatibu Tawala wa Wilaya (DAS) Tanzania bara yanayofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema ili viongozi hao waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo wanatakiwa waweke mikakati namba ambavyo wilaya zao ya zitakavyoweza wilaya kubeba na kusimamia vizuri ajenda za kitaifa.
”Hakikisheni mnadhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma katika maeneo yao na wanapobaini kuwepo kwa ubadhilifu wasisite kuchukua hatua.”amesema Waziri Mkuu
Hata hivyo amekemea migogoro kati yao na Wakuu wa Wilaya,mihemko na mienendo isiyofaa na kutaka wazingatie miiko na maadili ya viongozi wa umma.
“Wewe unataka ya kwako unasahau Mkuu wa Wilaya ndo kiongozi wa shughuli zote za serikali kwenye wilaya, wewe jukumu lako ni kumuwezesha yeye kutekeleza majukumu yake usipozingatia itifaki mtagombana kila siku kwasababu itifaki inakuzuia wewe kugombana na Mkuu wa Wilaya,”amesisitiza
Aidha Waziri Mkuu amewahimiza viongozi hao kusimamia tabia ya watumishi wa umma na kutunza siri za serikali.
“Tumeanza kuona nyaraka za siri za serikali zinakwenda mtandaoni huu nyie ndio mnapaswa kusimamia udhaifu huu,”amesema
Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea weledi viongozi hao ili kuimarisha utawala bora.
”Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Makatibu hao 135 na yalenga kuimarisha usimamizi wa utendaji kazi wao.”amesema Mhe.Simbachawene
Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angellah Kairuki, amewataka viongozi hao kutimiza majukumu yao ipasavyo na wahakikishe wanasimamia utekelezaji wa maagizo ya viongozi katika maeneo yao ya kazi.
Mafunzo hayo ya siku tatu yameandaliwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Taasisi ya Ungozi yamehusisha Makatibu Tawala wa Wilaya 135 za Tanzania Bara.