Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Dorice Mhimbira, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Walter MArick, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), mwenye shati jeupe Sohela Mabeyo, akizungumza wakati wa kutoa semina kwa watu wenye ulemavu wa kusikia namna ya kutumia huduma za mawasiliano na kuepukana na wizi wa mitandaoni, tukio lililofanyika jijini Dodoma.
Mmoja kati ya washiriki wa semina hiyo Yusuph Mloli, akiuliza swali kwa kutumia lugha ya vitendo kwa maafisa wa TCRA hawapo pichani, namna bora ya kutumia huduma ya mawasiliano wakati semina iliyofanyika jijini Dodoma.
Mmoja kati ya washiriki wa semina hiyo David Chamila, akiuliza swali kwa kutumia lugha ya vitendo kwa maafisa wa TCRA hawapo pichani, namna bora ya kutumia huduma ya mawasiliano wakati wa semina iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa semina walipokuwa wakiwasikiliza maafisa wa TCRA wakati wa semina ya kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu wa kusikia, namna bora ya kutumia huduma za mawasiliano, semina iliyofanyika jijini Dodoma.
…………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imekutana na kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu wa kutokusikia katika mkoa wa Dodoma kwa lengo la kutoa elimu kuhusu utumiaji wa huduma za mawasiliano na namna ya kukabiliana na changamoto katika kutumia huduma za mawasiliano.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo Afisa kitengo kinachoshughulika na wateja na watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka (TCRA), Walter Marick,amesema ni utaratibu wa mamlaka hiyo kutoa elimu ya mawasiliano kwa watumiaji, lakini watu hao wametoa maombi maalamu .
Kwa ajili ya kupatiwa mafunzo hayo kwa lengo la kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika kutumia bidhaa za mawasiliano, kwani watu hao wamekuwa wahanga katika kutumia mawasiliano kutokana na ulemavu walionao.
“Ni utaratibu kila wakati kutoa elimu kuhusu elimu ya kukabiliana na changamoto katika mawasiliano, lakini tumepewa ombi maalamu kwa ajili ya kutoa elimu kwa watu hawa wenye ulemavu wa kutokusikia, na elimu hii ni mahususi kwa sababu hawa ndio wahanga katika uhalifu wa mtandaoni”amesema Marick.
Amesema kundi hilo kama wadau wao wamekuwa na changamoto nyingi katika kutumia bidhaa za wasiliano, kwani baadhi yao hawana uelewa katika suala la changamoto za mawasiliano, hali inayopelekea kuathrika na vitendo vya wizi wa mitandaoni.
“Tumetoa tahadhari ya changamoto zilizopo katika mawasiliano ambazo wengi wamekuwa wakikutana nazo hasa katika utapeli, njia mojawapo wa kupunguza ni kumsaidia mtumiaji, mfano kapokea ujumbe wa kutakiwa kutuma fedha kwa namba usiyoifahamu usitekeleze kwanza na nini cha kufanya” amesema.
Aidha amesema na wao kama mamlaka wamesikia changamoto ambazo wanakutana nazo katika kutumia mawasiliano, na wengi hawana uelewa katika kukabiliana na vitendo vya wizi mitandaoni na uhalifu mwingine mitandaoni, hasa katika kutunza siri zao za mawasiliano kuepuka na na vitendo hivyo.
“Ametolea mfano baadhi yao wanaweza kuwa amejiunga kifurushi na kabla hajakitumia wakakata, na yeye bila kuelewa kuwa anahaki ya kujua, lakini ana amua kununua vocha na kujiunga tena bila kujua kwanini, na tumewaelekeza kuwa anapokutana na kitu kama hicho, anatakiwa kuhoji na tumewaelekeza mamlaka ilipo kwa ajili ya msaada zaidi anapokuwa hajaridhika na majibu ya mtoa huduma” amesema.
Pia amesema kila kanda kuna mamlaka za mawasiliano na wanajukumu la kuhakikisha wanatoa elimu kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano ili kila mtumiaji atambue haki yake katika kutumia huduma ya mawasiliano na namna ya kuepuka uhalifu wa mitandaoni.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwamo Yusuph Mloli na David Chamela, wenye ulemavu wa kusikia wameshukuru kupewa mafunzo hayo kwani yamekuwa msaada mkubwa kwao, na yametusaidia katika kuwafungua na kupata uelewa juu ya huduma za mawasiliano na mamna ya kukabiliana nazo.
“Niwashukuru sana TCRA kwa sababu hapo mwanzo sikuwa na uelewa na kunavitu nilikuwa na fanyiwa na mitandao ya simu lakini sikujua kama sitendewi haki lakini kwa sasa nimeelewa vizuri, na ukizingatia sisi watu wasioona ndio waathirika katika vitendo vya wizi mitandaoni” amesema Chamela.