*****************************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKOA wa Pwani umewathibitishia wawekezaji wanaowekeza kwenye mkoa huo kuwa mitaji yao italindwa kwani nchi ina amani na ni sehemu salama kwao.
Hayo yalibainishwa ,mjini Kibaha na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alipokuwa akizungumza na viongozi wawili wa serikali na wajumbe watatu chemba ya biashara kutoka Jimbo la Hebei nchini China walipotembelea maonyesho ya biashara za viwanda yanayofanyika wilayani Kibaha
Alisema kuwa ugeni huo ulikuja kwenye maonyesho hayo kwa ajili ya kuangalia kama wataweza kuwekeza na aliwahakikihia kuwa Tanzania ni nchi nzuri na ina usalama wa kutosha na mitaji yao itakuwa salama hivyo wasiwe na hofu juu ya usalama wa mitaji yao.
Ndikilo alieleza,wageni hao toka Hebei nchini China waliakwa kupitia kampuni ya Cpl inayomilikiwa kwa pmoja na raia wa China na raia wa Tanzania inayojihusisha na usagaji wa mahindi ili kupata unga kiwanda ambacho kiko wilayani Kibaha mkoani humo.
“Tumewahakikishia kuwa nchi yetu iko vizuri usalama wa kutosha na mitaji yao itakuwa salama kwani hata walipotembelea kwenye benki za NMB na CRDB wamethibitishiwa usalama wa mitaji yao endapo watakuja kuwekeza,” alisema Ndikilo.
“Jimbo la Hebei limeendelea kwenye viwanda vikiwemo vile vya vya simenti kwani walianza kuzalisha mnamo mwaka 1889 na linaongoza duniani kwa kuzalisha chuma ambapo moja ya tisa cha chuma duniani kinazalishwa kutoka jimbo hilo,” alisema Ndikilo
Wamewekeza kwenye nchi 90 duniani na Afrika wamewekeza kwenye nchi 27 na imewekeza miradi 127 nchi za kwenye nchi za Afrika kabla ya kuondoka wataangalia kwenye mwongozo wa uwekezaji wa mkoa .
“Hadi sasa jimbo la Hebei wamewekeza kwenye viwanda vitatu kwenye mkoa wa Pwani wamepita kwenye mabenki na kituo cha uwekezaji cha TIC na EPZA na wamefurahishwa sana na fursa zilizopo,” alisema Ndikilo.