Mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe Dkt Angeline Mabula amekabidhi viti kwa jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kata ya Ilemela kama sehemu ya kutimiza ahadi yake na juhudi katika kuimarisha chama chake
Akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ya viti 25 vilivyotolewa na kiongozi huyo, Ndugu Charles Karoli David ambae ni katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela MNEC Dkt Angeline Mabula amesema kuwa Mhe Dkt Mabula ni kiongozi wa vitendo anaeyaishi maneno yake hivyo wananchi waendelee kumuunga mkono na kushirikiana nae katika kutekeleza shughuli za maendeleo
‘.. Mbunge wetu ni mtu wa vitendo aliahidi na leo ametekeleza ahadi yake, Na sio viti tu shughuli za maendeleo kila kukicha zinaendelea ndani ya jimbo letu ..’ alisema
Aidha Ndugu Karoli ametaja miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan ndani ya wilaya ya Ilemela ikiwemo ya sekta za afya, elimu, miundombinu na maji sambamba na kuwaasa wananchi kuendelea kumuombea Rais Dkt Samia na Serikali yake
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ilemela Bi Salome Kipondya amemshukuru Mbunge huyo Kwa moyo wake wa kujitoa katika kuwahudumia wananchi wa jimbo lake pamoja na kuahidi ushindi kwa nafasi za Urais, ubunge, udiwani na Serikali za mitaa Kwa kuwa kazi kubwa ya maendeleo imefanyika na inaendelea
Winfrida Gyunda ni diwani wa viti maalum kutoka kata ya Buswelu ambae pia ni mlezi wa kata ya Ilemela ambapo mbali na kumpongeza Mbunge huyo Kwa kazi kubwa ya Utekelezaji wa miradi ya maendeleo amekuwa akishikamana na wananchi wake katika maendeleo kwa wananchi kuanzisha miradi katika hatua za misingi, Mbunge kutoa tofali za ujenzi wa mradi huo katika hatua za kunyanyua boma na kisha Serikali kukamilisha
Nae Bi Tabu Tito ambae ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake UWT kata ya Ilemela amemshukuru Mbunge MNEC Mhe Dkt Angeline Mabula kwa msaada huo wa viti kwani jumuiya yake ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya kukaa chini wakati wa utekelezaji wa shughuli zake za kila siku jambo lililokuwa likikwamisha kuimarika Kwa chama hicho na kusonga mbele
MNEC Dkt Angeline Mabula amekuwa na desturi ya kugawa vifaa kama sehemu ya kuimarisha chama na jumuiya zake, kusaidia upatikanaji wa mitaji ya utekelezaji wa shughuli za kiuchumi sanjari na kutoa elimu ya ujasiriamali na kujikwamua kiuchumi kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu