Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu),
Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa
wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata
yaliyoanza leo Juni 19,2023 jinini Tanga. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni
maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika
tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata yaliyoanza leo Juni 19,2023 jinini Tanga. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.
Washiriki wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata yaliyoanza leo Juni 19,2023 jinini Tanga. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.

Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Balozi Omar Ramadhan Mapuri akisalimia wakati wa mkutano huo wa mafunzo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe akizungumza.
Wilaya ya Tanga, Mh. Ruth Mkisi akiwaongoza wasimamizi wa Uchaguzi na
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata kula kiapo cha kujitoa
uanachama wa vyama vya siasa na kiapo cha kutunza siri.
ya wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na
Kata wakila kiapo cha kujitoa unachama wa vyama vya siasa na kiapo cha kutunza
siri kabla ya kuanza kwa mafunzo ya siku tatu yaliyoanza jana jijini Tanga. Mafunzo
hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata 14 za Tanzania
Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za
madiwani.
Baadhi

Na Mwandishi Maalum, Tanga.
Uchaguzi wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia Katiba, Sheria,
Kanuni na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wote wanapotekeleza
majukumu yao.
Hayo yamesemwa
na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya
Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa Wasimamizi na
Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata leo tarehe 19 Juni, 2023
jijini Tanga.
yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa kata 14 za Tanzania Bara
unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.
mnalotakiwa kuzingatia ni kujiamini na kufanya kazi kwa weledi, mnapaswa kuzingatia
Katiba ya Nchi, Sheria za Uchaguzi na Kanuni zake, Maadili ya Uchaguzi na
Maelekezo mbalimbali yanayotolewa na yatakayotolewa na Tume katika kipindi hiki
cha uchaguzi mdogo,” amesema Jaji Mbarouk.
Amewaasa
washiriki hao wa mafunzo kuhakikisha kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yao
wanao katika uendeshaji wa uchaguzi, wahakikishe wanazingatia maelekezo watakayopewa
na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea.
“Uchaguzi ni
mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kisheria ambazo hupaswa
kufuatwa na kuzingatiwa, hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi kuwa
mzuri, wenye ufanisi na kupunguza kama siyo kuondoa kabisa malalamiko au vurugu
wakati wote wa mchakato wa uchaguzi,” amesema Jaji Mbarouk.
Amewataka
watendaji hao wa uchaguzi kuvishirikisha vyama vya siasa na wadau wengine wa
uchaguzi katika maeneo yao kuhusu masuala mbalimbali ya kiuchaguzi ambayo
wanastahili kushirikishwa ili kurahisisha utendaji wa kazi.
Jaji Mbarouk
amewaelekeza wasimamizi hao wa uchaguzi kuhakikisha kuwa watendaji wa vituo vya
kupigia kura ni watu wenye weledi na uwezo mkubwa na kuweka utaratibu mzuri
utakaowezesha vituo kufunguliwa saa 1:00 asubuhi siku ya kupiga kura.
Kata
zilizotarajiwa kufanya uchaguzi mdogo ni pamoja na Ngoywa iliyopo Halmashauri
ya Wilaya ya Sikonge, Kalola iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Sindeni
iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Potwe iliyopo Halmashauri Manispaa ya
Muheza, Kwashemshi iliyopo Halamshauri ya Wilaya ya Korogwe, Bosha iliyopo
Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Mahege iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Kibiti na Bunamhala iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Nyingine ni,
Njoro na Kalemawe zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Same, Mnavira
iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kinyika iliyopo katika
Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Magubike iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya
ya Kilosa na Mbede iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.