Wananchi mbalimbali wakipata huduma za kuangalia afya katika maadhimisho ya siku ya sikoseli ambayo huadhimishwa kila ifika juni 19 Duniani kote Huko Skuli ya Maandalizi Kidutani Mjini Unguja,
Mfamasia Juma Rashid Hassein akisoma risala ya watoto wenye ugonjwa wa mifupa (sickel cell) wakati wakiadhimisha siku ya Sikoseli Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Juni 19,hafla iliyofanyika skuli ya maandalizi Kidutani Mjini Unguja juni 18.2023
Shujaa Hajji Ally Issa akitoa elimu fupi kuhusiana na ugonjwa wa sikoseli (SCD) wakati wa maadhimisho ya siku ya ugonjwa huo ambayo huadhimishwa kila ifikapo Juni 19 Duniani kote ,hafla iliyofanyika Skuli ya Maandalizi Kidutani.
Mkurugenzi Tiba Hospitali ya Mnazimmoja Dkt.Marijani Msafiri akizungumza machache na kumkaribisha mgeni Rasmi Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui kuzungumza na wazazi wa watoto wenye ugonjwa wa mifupa (SICKEL CELL) wakati wakiadhimisha siku ya ugonjwa huo ambao huadhimishwa kila ifikapo juni 19 Duniani kote ,hafla iliyofanyia Skuli ya Maandalizi Kidutani
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na madaktari pamoja na wazazi wa watoto wenye ugonjwa wa mifupa (SICKEL SELL) katika maadhimisho ya siku ya sikoseli Duniani ambayo haudhimishwa kila ifikapo juni 19,hafla iliyofanyika Skuli ya Maandalizi Kidutani.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye ugonjwa wa sikoseli katika maadhimisho ya siku ya ugonjwa huo amabayo huadhimishwa kila ifikapo juni 19.hafla iliyofanyika Skuli ya Maandalizi Kidutani.PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Na fauzia Mussa Maelezo
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Wizara inakusudia kuweka kliniki maalum za wagonjwa wa mifupa (SICKEL CELL) katika hospitali za Wilaya ili kupunguza changamoto ya kufuata huduma hizo katika hospitali ya Mnazimmoja.
Ameyasema hayo wakati akipokua akizungumza na madaktari pamoja na wazazi wa watato wenye ugonjwa huo katika maadhimisho ya siku ya sikoseli yaliofanyika Skuli ya maandalizi Kidutani Mjini Unguja.
Alisema kwa sasa zanzibar ina wagonjwa zaidi ya mia mbili wanaojulikana wa sikoseli hivyo hatua ya kuanzishwa kliniki katika hospitali za Wilaya kutawapunguzia mzigo Hospitali ya Mnazimmoja na kuwaacha wakihudumia wagonjwa walioshindikana katika hospitali za Wilaya na Mkoa.
Akizungumizia suala la upatikanaji wa damu salama ambayo ndio hitajio kubwa la wagonjwa hao Waziri mazrui alisema upatikanaji wa damu bado ni mdogo kulingana na mahitaji hivyo ameitaka jamii kujitokeza na kushajihishana kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu hasa watoto wanaoishi na ugonjwa wa mifupa kwani wao ndio wahitaji wakubwa.
“Ipo haja sasa ya kuchangishana damu kama tunavyochangishana katika mambo mengine ili tuokoe maisha ya wagonjwa wa sikoseli na kujiwekea akiba sisi wenyewe kwani pia niwahitaji watarajiwa.” Alisisitiza Waziri Mazrui
Mapema Waziri mazurui aliutaka Uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja kuhakikisha maadhimio waliojiwekea yanatimia ikiwemo kujenga na kuimarisha jumuiya za kilimwengu za seli mundu pamoja na kurasimisha uchunguzi wa watoto wachanga wanapozaliwa ili kujua Hali ya ugonjwa wa sikoseli.
Alifahamisha kuwa maadhimisho hayo yanafanyika si kwaajili ya kufurahia uwepo wa ugonjwa huo Bali ni kwa ajili ya kujuana , kuweka na kusimamia mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Katika kuhakikisha watoto hao wanatambulika na kupata misaada mbalimbali Waziri Mazrui aliwataka Madaktari kwa kushirikiana na wazazi wa watoto hao kuanzisha jumuiya maalum ili kuweza kutambulika na kupata misaada mbalimbali kutoka kwa wafadhili wa nje na ndani ya nchi.
“Kipimo kimoja cha kupima selimundu kwa mtoto mchanga kinagharimu elfu13 , tukiwa na jumuiya kutapelekea kupata Misaada angalau wa hivi vipimo vya kuchunguzia ugonjwa huu kwa watoto wetu mara tu wanaozaliwa kama tunavyowachunguza virusi vya ukimwi” alishauri waziri mazurui.
vile vile aliwataka wanandoa watarajiwa kuchunguza afya zao kwa kuangalia hali ya sikoseli kabla ya ndoa kwani endapo wazazi watakua na ugonjwa huo Wana nafasi kubwa ya kurithisha kizazi kitakachozaliwa .
“Tuache kuendekeza mapenzi ifike wakati tuchunguzane sikoseli kama tunavyochunguzana ukimwi kabla ya ndoa,hii itasaidia kupungua kwa watoto wanaorithishwa sikoseli kutoka kwa wazazi wao” alisisitiza Mazurui
sambamba na hayo Waziri Mazrui aliwashukuru madaktari kwa kuwapatia huduma bora watoto hao pamoja na wazazi wanaoendelea kuwatunza kwani kuna baadhi ya wazee huwatelekeza mara baada ya kugundua ni wagonjwa.
Nao wazazi wa watoto wanaoishi na ugonjwa huo Wameiomba Wizara kutowakuwachanganya watoto wao katika wodi ya watu wazima wafikapo umri wa miaka 13 kwani bado ni wadogo na wanahitaji kuwa karibu na wazazi.
Aidha waliushauri Uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja kuweka wodi maalum kwaajili ya watoto wenye ugonjwa huo wenye umri wa kuanzia miaka 13 Hadi 18 ili waweze kuwa nao karibu katika kipindi kigumu cha ugonjwa.
Dunia huadhimisha siku ya Ugonjwa wa SICKEL CELL kila ifikapo Juni 19 kwa lengo la kuwajengea uelewa na kufanya ukaguzi wa afya kwa watu mbali mbali ili kuchukua tahadhari za mapema juu ya ugonjwa huo,
Kauli mbiu “VUNJA MDUARA,PIMA JUWA HALI YAKO YA SIKOSELI”